Falsafa ya Kiafrika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Falsafa ya Kiafrika inaweza kumaanisha falsafa ya wasomi Waafrika, au falsafa inayopendekeza mtazamo wa Waafrika, au falsafa inayotumia mbinu maalumu za Kiafrika.[1][2]

Kabla ya Uzodinma Nwala kuanza kufundisha somo hilo, hakukuwa na chuo kikuu chochote kilicholifundisha.[3]

Falsafa ya Kiafrika inaweza kufafanuliwa kama hoja za Waafrika juu ya mang'amuzi ya maisha yao. [4]

Hiyo ilikuwepo hata kabla ya ukoloni uliowakutanisha na falsafa ya Magharibi.[5]

Hasa Misri ya Kale iliwahi sana kuwa na falsafa yenye utajiri wa mawazo, halafu ikachangia falsafa ya Kigiriki na falsafa ya Kikristo.

Katika karne ya 20 tapo la kupinga ukoloni Afrika lilichochea hasa falsafa ya kisiasa ambayo ilipata maitikio makubwa ndani na nje ya bara hilo, ikichochea juhudi za ukombozi sehemu nyingi. Mfano mmojawapo ni falsafa ya Ujamaa iliyozaliwa na Julius Nyerere nchini Tanzania.

Orodha ya wanafalsafa Waafrika[hariri | hariri chanzo]

Afrika Kusini
Algeria
Benin
Ethiopia
Falsafa ya Kigiriki
Ghana

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Kamerun
Kenya
Libya
Misri

Moroko
Nigeria
Rwanda
Senegal
Tanzania
Tunisia
Zimbabwe

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Bruce B. Janz, Philosophy in an African Place (2009), pp. 74-79, Plymouth, UK: Lexington Books, https://books.google.com/books?isbn=0739136682
  2. Samuel Oluoch Imbo, An Introduction to African Philosophy (1998), pp. 38-39, https://books.google.com/books?isbn=0847688410
  3. "All we were taught as students were Western philosophy. Nothing like African philosophy existed anywhere. In fact, many years after the introduction of the courses, there still remained arguments among experts, whether there was really African Philosophy".
  4. Nigerian born Philosopher K.C. Anyanwu defined African philosophy as "that which concerns itself with the way in which African people of the past and present make sense of their destiny and of the world in which they live." Peters, R.S. (1959). Authority, Responsibility and Education. London: G. Allen & Unwin. 
  5. Nigerian philosopher Joseph I. Omoregbe broadly defines a philosopher as one who attempts to understand the world's phenomena, the purpose of human existence, the nature of the world, and the place of human beings in that world. This form of natural philosophy is identifiable in Africa even before individual African philosophers can be distinguished in the sources. Maurice Muhatia Makumba, An Introduction to African Philosophy: Past and Present (2007), p. 25, https://books.google.com/books?isbn=9966082964

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]