Michezo ya Afrika Nzima

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lagos 1973

Michezo ya Afrika Nzima (pia huitwa Michezo ya Afrika au Michezo ya Pan Afrika) ni tukio la michezo mbalimbali ya mataifa ya Afrika linalofanyika kila baada ya miaka minne, linaloandaliwa na Muungano wa Kamati za Kitaifa za Olimpiki za Afrika (ANOCA). Mataifa yote yanayoshiriki lazima yawe ya bara la Afrika.

Tukio la kwanza lilifanyika mwaka wa 1965 katika mji wa Brazzaville, nchini Jamhuri ya Kongo. Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) ilitoa utambulisho rasmi kwa tukio hilo kama tukio la bara la michezo mbalimbali, sambamba na michezo ya Pan American na Michezo ya Bara la Asia.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mwanzilishi wa Olimpiki ya kisasa Pierre de Coubertin alianzisha michezo ya Pan African mapema mwaka wa 1920. Mamlaka za kikoloni zilizokuwa zinatawala Afrika wakati huo zilikuwa zinahofia wazo hilo, zikishuku kuwa umoja wa Waafrika kwa njia ya mchezo kungesababisha Waafrika kudai uhuru wao.

Majaribio yalifanywa ili kuandaa michezo hiyo Algiers, nchini Algeria, na Alexandria, nchini Misri, miaka 1925 na 1928, lakini licha ya maandalizi kabambe yaliyofanywa na waratibu, juhudi hizo zilitumbukia nyongo. Mwanachama wa kwanza kutoka Afrika wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, mwanariadha wa masafa mafupi aliyezaliwa nchini Ugiriki mwenye uraia wa Misri, Angelo Bolanaki, alichangia fedha kujengwe uwanja, lakini michezo haikufanyika hadi baada ya miongo mingine mitatu.

Katika miaka ya mapema ya 1960, nchi za Afrika zilizokuwa zinazungumza Kifaransa zilipanga Michezo ya Urafiki. Michezo hiyo ilipangwa na Madagascar (1960) na kisha Côte d'Ivoire (1961). Michezo ya tatu ilipangwa kufanyika nchini Senegal mwaka wa 1963.

Kabla ya michezo hiyo kukamilika, Mawaziri wa Vijana na Mchezo wa Kiafrika walikutana Paris mwaka wa 1962, na kwa sababu chache za nchi zilizokuwa zinazungumza Kiingereza zilikuwa tayari zinashiriki, wao wakaipa Michezo hiyo jina la Michezo ya Pan Africa. Michezo hiyo ilipewa utambulisho rasmi na IOC kuwa katika kiwango sawa na michezo mingine ya kibara kama vile michezo ya bara Asia na Michezo ya Pan America.

Mnamo Julai mwaka wa 1965, toleo la kwanza lilifanyika Brazzaville, nchini Congo, sasa ikijulikana kama michezo ya All-Africa. Kutoka mataifa 30, idadi ya wanariadha karibu 2500 walishiriki. Misri ilishikilia nafasi ya kwanza kwa kupata idadi kubwa ya medali.

Katika mwaka wa 1966, Kamati Kuu ya Michezo katika Afrika (SCSA) ilipangwa mjini Bamako; inasimamia michezo ya All-Africa. Toleo la pili lilituzwa nchi ya Mali katika mwaka wa 1969, lakini mapinduzi ya kijeshi yalilazimisha kufutiliwa mbali kwa Michezo hiyo. Lagos, Nigeria ilijitolea kuwa mwenyeji wa michezo hiyo mwaka wa 1971. Hatimaye michezo hiyo ilifanyika mwaka wa 1973 kutokana na Vita vya Biafra, ambavyo vilikuwa vimekwisha karibuni nchini Nigeria.

Katika mwaka wa 1977, toleo la 3 la michezo hiyo lilikuwa limepangwa kufanyika nchini Algeria, lakini kutokana na sababu za kiufundi, yaliahirishwa kwa muda wa mwaka moja na yalifanyika mwaka wa 1978.

Kwa kuendeleza mtindo huo, toleo lililofuata lilipangwa kufanyika nchini Kenya mwaka wa 1983, lakini lilisogezwa hadi mwaka wa 1985 na hatimaye yalifanyika mjini Nairobi mwaka wa 1987.

Mtindo wa Olimpiki wa miaka minne haujakosa kufuatwa, na michezo hiyo imepangwa Cairo, Harare, Johannesburg, na Lagos. Katika mwaka wa 2007, Algiers kwa mara nyingine tena ilikuwa mwenyeji wa michezo na kuwa ya kwanza kurudia uenyeji wa michezo hii. Lusaka nchini Zambia imejiondoa (mnamo Desemba 2008) kama mwenyeji wa toleo lijalo la michezo hiyo mwaka wa 2011.

Miji wenyeji wa michezo hii[hariri | hariri chanzo]

Orodha Mwaka Jiji Nchi Tarehe Nchi yenye medali nyingi
1 1965 Brazzaville Bendera ya Jamhuri ya Kongo Congo-Brazzaville 18 Julai - 25 Julai 1965 Bendera ya United Arab Republic United Arab Republic
-- 1969 Bamako Bendera ya Mali Mali Ulikatizwa kutokana na mapinduzi ya kijeshi
2 1973 Lagos Bendera ya Nigeria Nigeria 7 Januari - 18 Januari 1973 Bendera ya Misri Egypt
3 1978 Algiers Bendera ya Algeria Algeria 13 Julai - 28 Julai 1978 Bendera ya Tunisia Tunisia
4 1987 Nairobi Bendera ya Kenya Kenya 1 Agosti - 12 Agosti 1987 Bendera ya Misri Egypt
5 1991 Cairo Bendera ya Misri Egypt 20 Septemba - 1 Oktoba 1991 Bendera ya Misri Egypt
6 1995 Harare Bendera ya Zimbabwe Zimbabwe 13 Septemba - 23 Septemba 1995 Bendera ya Afrika Kusini South Africa
7 1999 Johannesburg Bendera ya Afrika Kusini South Africa 10 Septemba - 19 Septemba 1999 Bendera ya Afrika Kusini South Africa
8 2003 Abuja Bendera ya Nigeria Nigeria 5 Oktoba - 17 Oktoba 2003 Bendera ya Nigeria Nigeria
9 2007 Algiers Bendera ya Algeria Algeria 11 Julai - 23 Julai 2007 Bendera ya Misri Egypt
10 2011 Maputo Bendera ya Msumbiji Mozambique 15 Julai - 27 Julai 2011

Mji utakaokuwa mwenyeji wa makala ya 2015 ya michezo hii utaamuliwa hivi karibuni. Accra, Ghana na Kenya zimetajwa kama zenye uwezekano wa kuwa wenyeji.

Orodha ya medali[hariri | hariri chanzo]

Orodha inayofuata inaonyesha medali zilizohesabiwa katika matukio yote ya michezo hii.

Nafasi Nchi Dhahabu Fedha Shaba -Jumla Mwaka wa
medali ya kwanza
1 Bendera ya Misri Misri 431 328 320 1079 1965
2 Bendera ya Nigeria Nigeria 303 277 256 836 1965
3 Bendera ya Afrika Kusini Afrika Kusini 198 174 137 509 1995
4 Bendera ya Algeria Algeria 132 152 189 473 1965
5 Bendera ya Tunisia Tunisia 123 [85] 133 362 1965
6 Bendera ya Kenya Kenya 90 97 104 291 1965
7 Bendera ya Senegal Senegal 40 40 73 153 1965
8 Bendera ya Ghana Ghana 26 38 64 128 1965
9 Bendera ya Ethiopia Ethiopia 23 29 34 86 1965
10 Bendera ya Kamerun Cameroon 20 42 81 143 1965
11 Bendera ya Zimbabwe Zimbabwe 18 26 57 101 1987
12 Bendera ya Uganda Uganda 17 19 33 69 1965
13 Bendera ya Côte d'Ivoire Côte d'Ivoire 17 18 33 68 1965
14 Bendera ya Madagaska Madagascar 10 15 33 58 1965
15 Bendera ya Moroko Moroko 9 12 15 36 1973
16 Bendera ya Angola Angola 9 7 17 33 1987
17 Bendera ya Lesotho Lesotho 8 3 8 19 1991
18 Bendera ya Morisi Mauritius 6 19 27 52 1987
19 Bendera ya Libya Libya 6 8 16 30 1978
20 Bendera ya Namibia Namibia 4 10 15 29 1991
21 Bendera ya Tanzania Tanzania 4 8 10 22 1965
22 Bendera ya Zambia Zambia 4 4 22 30 1965
23 Bendera ya Mali Mali 4 4 7 16 1965
24 Bendera ya Gabon Gabon 4 4 19 27 1965
25 Bendera ya Botswana Botswana 4 4 10 18 1991
26 Bendera ya Msumbiji Mozambique 4 2 [1] 7 1987
27 Bendera ya Eritrea Eritrea 3 [1] 2 6 2007
28 Bendera ya Sudan Sudan 3 [1] 3 7 1973
29 Bendera ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Democratic Republic of the Congo 2 3 6 11 1965
30 Bendera ya Jamhuri ya Kongo Republic of the Congo [1] 7 15 23 1965
31 Bendera ya Jamhuri ya Afrika ya Kati Central African Republic [1] 2 2 5 1991
32 Bendera ya Guinea Guinea [1] 2 [1] 4 1973
Bendera ya Sierra Leone Sierra Leone [1] 2 [1] 4 1991
33 Bendera ya Eswatini Eswatini [1] 0 9 10 1973
34 Bendera ya Chad Chad [1] 0 9 10 1965
35 Bendera ya Cabo Verde Cape Verde [1] 0 2 3 1999
36 Bendera ya Burkina Faso Burkina Faso [1] 0 [1] 2 1987
37 Bendera ya Somalia Somalia [1] 0 0 [1] 1973
38 Bendera ya Shelisheli Seychelles 0 13 18 31 1987
39 Bendera ya Burkina Faso Burkina Faso 0 3 7 10 1965
40 Bendera ya Togo Togo 0 2 10 12 1965
41 Bendera ya Niger Niger 0 2 6 8 1965
42 Bendera ya Benin Benin 0 2 3 5 1973
43 Bendera ya Gambia Gambia 0 2 0 2 1973
44 Bendera ya Rwanda Rwanda 0 2 0 2 1987
45 Bendera ya São Tomé na Príncipe São Tomé and Príncipe 0 [1] [1] 2 2003
46 Bendera ya Malawi Malawi 0 0 2 2 1987
47 Bendera ya Guinea-Bisau Guinea-Bissau 0 0 [1] [1] 1999

Ushawishi[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kusikia kuhusu michezo ya Pan-Afrika wakati akiwa katika ziara za kibiashara huko Kongo, mwanadiplomasia Mrusi - Muarmenia Ashot Melik-Shahnazaryan alipata wazo la kuanzisha michezo ya Pan-Armenia.

Angalia Pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]