Ubuntu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ubuntu (falsafa))
Sanamu ya tembo yenye mchoro wa Ubuntu, Florianópolis, Brazil

Ubuntu ni falsafa ya Kiafrika inayosisitiza mahusiano na ushirikiano wa jamii kama msingi wa maisha bora na amani katika jamii. Falsafa hii inaonesha nafasi ya mtu katika jamii iliyomzunguka. Ushirikiano ni njia bora ya kuishi kama jamii kuliko ubinafsi.

Neno Ubuntu limetoka kwenye lugha za Kizulu na Kixhosa za Afrika Kusini. Neno la Kihaya "Obuntu" au kwa Kiswahili "utu" linabeba, kwa kiasi fulani, maana ya neno Ubuntu.

Falsafa ya Ubuntu imetokana na mila na utamaduni wa Kiafrika ambao umejengwa juu ya maslahi ya jamii zaidi ya maslahi ya mtu binafsi.

Msingi wa falsafa hii ni, "mtu si mtu bila watu," kwa Kizulu, "Umuntu ngumuntu ngabantu." Kwa Kihaya "Omuntu ti muntu ka ataliho bantu" Baadhi ya watu wanaiona falsafa ya Ubuntu kuwa na maana nzito ya kiroho na ya kidini kwa kuwa imejengwa juu ya upendo wa watu wengine (kama unavyojipenda wewe) na hata mazingira.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ubuntu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.