Kizulu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Shujaa wa kabila la Zulu

Kizulu (isiZulu) ni lugha ya Wazulu inayoongelewa nchini Afrika Kusini, na idadi ya watu wanaokadiriwa kuwa milioni 9-10 hasa katika jimbo la KwaZulu-Natal. Kizulu huhesabiwa kati ya lugha za Kinguni ndani ya lugha za Kibantu.

Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kizulu nchini Afrika Kusini imehesabiwa kuwa watu 9,980,000. Pia kuna wasemaji nchini Botswana, Lesotho, Malawi, Msumbiji na Uswazi. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kizulu iko katika kundi la S40.

Wakati wa mfecane katika karne ya 19 wasemaji wa lugha ya Kizulu zimehama hadi Zimbabwe, Zambia, Msumbiji na Tanzania ambapo lugha imebadilika kiasi kikubwa kwa mfano Kindebele au Kingoni.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Noun project 1822.svg Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kizulu kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.