Kiwolofu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kiwolofu

Kiwolofu ni lugha iongewayo nchini Senegal, Gambia, na Mauritania. Ni lugha rasmi kwa Wawolofu. Lugha hii ipo kama lugha jirani ya Fula inayohesabiwa kati ya lugha za Kiatlantiki cha familia ya lugha za Niger-Kongo.

Kiwolofu ni lugha inayoongelewa sana nchini Senegal, haizungumzwi na Wawolofu tu (karibuni asilia 40 ya watu huzungumza kama lugha ya mama) bali hata Wasenegal wengine huzumgumza lugha hii. Lahaja za Kiwolofu zaweza kufanana sana kati ya nchi hizi mbili, yaani Senegal na Gambia, zikiwa sambamba kabisa kitabia na hata kuongelewa kieneo.

Idadi ya wasemaji kama lugha ya mama ni takriban milioni 3.2 na karibu idadi ileile hutumia Kiwolofu kama lugha ya pili.

Kuna lahaja mbalimbali kama vile "Dakar-Wolof". Dakar ni mji wenye watu mchanganyiko, yaani kunawaongeaji wa Kiwolofu, Kifaransa, Kiarabu, na hata Kiingereza huzungumzwa kidogo pia katika mji huo wa Dakar, mji ambao uko nchini Senegal.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Noun project 1822.svg Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kiwolofu kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.