Nouakchott
Jiji la Nouakchott | |
Nchi | Mauritania |
---|
Nouakchott (Kiarabu: نواكشوط) ni mji mkuu wa Mauritania. Iko mwambaoni wa Atlantiki katika magharibi ya nchi. Idadi ya wakazi imekadiriwa kupita milioni moja.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Hadi 1958 Nouakchott ilikuwa kijiji kidogo cha wavuvi. Imekua tangu uhuru. Wakati wa ukoloni Mauretania haikuhesabiwa kama eneo la pekee ilikuwa sehemu tu ya Afrika ya Magharibi ya Kifaransa yenye mji mkuu wa Saint-Louis huko Senegal.
Baada ya azimio la kupasua eneo la Kifaransa katika Afrika ya Magharibi Nouakchott ikateuliwa kuwa mji mkuu ujao na mradi wa ujenzi ulilenga kuongeza idadi ya wakazi hadi kufikia watu 15,000. Baada ya uhuru mwaka 1962 mji ukawa mji mkuu wa Mauretania.
Katika miaka ya 1970 idadi ya wakazi iliongezeka sana kutokana na ukame uliofukuza watu wengi mashambani, kati ya 1969 na 1980 kutoka wakazi 20,000 kufikia 150,000 mwaka 1980.
Siku hizi mju una tatizo zito ya uhaba wa maji kwa wakazi wake wengi.