Nenda kwa yaliyomo

KwaZulu-Natal

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mkoa wa Zulu-Natal
KwaZulu-Natal
Eneo 92,100 km²
Wakazi(2001) 9,426,019
Lugha Kizulu (80.6%)
Kiingereza (13.6%)
Kixhosa (2.3%)
Kiafrikaans (1.5%)
Wakazi kimbari Waafrika Weusi(85.3%)
Wenye asili ya Asia (8.5%)
Wazungu(4.7%)
Chotara(1.5%)
Mji Mkuu Pietermaritzburg
’‘‘Mji Mkubwa’’’ Durban
Waziri Mkuu S'bu Ndebele
(ANC)
Mahali pa KwaZulu-Natal
Ramani ya KwaZulu-Natal

KwaZulu-Natal ni moja kati ya majimbo tisa ya Afrika Kusini. Imepakana na Eswatini, Msumbiji, Lesotho, Bahari Hindi na majimbo ya Afrika Kusini ya Mpumalanga, Rasi ya Mashariki na Dola Huru. Jimbo liliundwa 1994 kwa kuunganisha jimbo la Natal na bantustan ya KwaZulu. Mji mkuu ni Pietermaritzburg.

Demografia na utamaduni[hariri | hariri chanzo]

KwaZulu-Natal ni jimbo la Afrika Kusini lenye wakazi wengi waliohesabiwa mwaka 2001 walikuwa milioni tisa na nusu. Ni hasa eneo la Wazulu lakini ni pia jimbo lenye wakazi wengi wenye asili ya Asia hasa Uhindi.

Lugha inayozunguzwa zaidi ni Kizulu halafu Kiingereza.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Eneo la jimbo ni 92 100 km2. KwaZulu-Natal iko upande wa mashariki wa Afrika Kusini ina pwani ndefu la Bahari Hindi. Uso wa nchi unapendeza hivyo jina la "Jimbo la Bustani".

Kuna kanda tatu:

  • tambarare ya pwani
  • nyanda za vilima
  • milima ya juu ambayo ni milima ya Drakensberg upande wa magharibi na milima ya Lebombo upande wa kaskazini. Katika sehemu kubwa ya jimbo hali ya hewa ni ya joto lakini kwenye nyanda za juu na mlimani kuna vipindi vya baridi.

Hali joto ni kati ya 17 °C hadi 28 °C kati ya Oktoba na Aprili halafu kati ya 11° hadi 25 °C wakati wa baridi. Mvua hunyesha takriban 690 mm kwa mwaka.

Mto mkubwa unaovuka jimbo ni mto Tugela.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Durban ni bandari kuu ya Afrika Kusini na kitovu cha viwanda vingi. Bandari ya Richards Bay inatumiwa hasa kwa kubeba nje makaa mawe kuna pia kiwanda kikubwa cha aluminiamu. Migodi ya makaa mawe yako hasa Vryheid, Dundee, Glencoe na Newcastle.

Sehemu muhimu wa uchumi ni utalii ya pwani.

Kilimo cha pwani ni hasa ya miwa lakini pia ya matunda. Kilimo cha bara kuna pia mboga na ufugaji.


Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu KwaZulu-Natal kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.