Durban
Jiji la Durban | |
Mahali pa mji wa Durban katika Afrika Kusini |
|
Majiranukta: 29°52′12″S 30°59′24″E / 29.87000°S 30.99000°E | |
Nchi | Afrika Kusini |
---|---|
Majimbo | KwaZulu-Natal |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 3 468 086 |
Tovuti: www.durban.gov.za |
Durban ni mji wa Afrika Kusini katika jimbo la KwaZulu-Natal. Kuna takriban wakazi milioni 4 . Fuko za Durban zapendwa na watalii kwa sababu maji ya Bahari Hindi si baridi na kuna jua tele. Bandari ya mji ni kubwa katika Afrika Kusini ni bandari asilia duniani yenye kina kikubwa.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Habari za kwanza za Durban zimepatikana kutoka kwa mpelelezi na mbaharia Mreno Vasco da Gama aliyefika hapa 25 Desemba 1497. Aliita mahali Rio de Natal au "mto wa Krismasi" kutokana na tarehe ya kufika kwake. Hii ni chanzo cha jina "Natal" kwa ajili ya jimbo.
Mji ulianzishwa 1824 na kikosi cha wanajeshi Waiingereza waliojenga makazi kwenye pwani la hori ya Natal. Mmoja wao aliweza kumsaidia mfalme wa Zulu Shaka aliyegonjeka kutokana na majeruhi. Mfal,me akatoa shukrani kwa kumpa Mwingereza zawadi ya kanda la eneo lenye urefu wa maili 25 kwenye pwani na upana wa maili 100 kuingia bara. Mji uliitwa kwa heshima wa gavana wa koloni ya Rasi Sir Benjamin d'Urban hivyo "Durban".
Katika karne ya 19 Waingereza walichukua wafanyakazi wengi kwa ajili ya mashamba ya miwa kutoka Bara Hindi ambao ni chanzo cha wakazi Waasia wa Durban. Kati ya 1893 na 1915 Durban ilikuwa mahali ambapo Mahatma Gandhi alifanya kazi kama mwanasheria.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti rasmi Ilihifadhiwa 29 Machi 1996 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika Kusini bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Durban kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |