Koloni ya Rasi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Cape Colony - Kaapkolonie
Koloni ya Rasi
Bendera ya Koloni ya Rasi
Lugha rasmi Kiingereza na Kiholanzi 1
Mji mkuu Cape Town
Eneo 569,020 km² (1910)
Koloni ya Rasi katika Muungano wa Afrika Kusini
1 Hadi 1806 Kiholanzi ilikuwea lugha rasmi pekee; kati ya 1806 na 1882 Kiingereza. Tangu 1882 lugha zote mbili zilikuwa lugha rasmi.

Koloni ya Rasi ilikuwa koloni ya Uholanzi hadi 1806 na baadaye ya Uingereza katika Afrika Kusini ya leo. Jina limetokana na Rasi ya Tumaini Jema iliyoko karibu na mji wa Cape Town.

Koloni ya Uholanzi[hariri | hariri chanzo]

Historia ya koloni ilianza 1652 wakati Mholanzi Jan van Riebeeck aliunda Cape Town kwa niaba ya Kampuni ya Kiholanzi kwa India ya Mashariki. Kampuni ilihitaji kituo kwa ajili ya jahazi zake zilizosafiri kati ya Ulaya na visiwa vya Indonesia. Eneo la rasi lilifaa kuwa mahali pa kupumzika na kuongeza vyakula njiani tena kwa sababu hali ya hewa iliwafaa watu wa Ulaya.

Waholanzi walipeleka wakulima kwenda rasi waliotakiwa kulima vyakula kwa ajili ya mahitaji ya jahazi.

Koloni ya Uingereza[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa vita za Napoleoni eneo la Uholanzi lilitawaliwa na Ufaransa na Uingereza ilivamia koloni za Uholanzi pamoja na rasi. Waingereza waliogopa ya kwamba Wafaransa wangehatarisha mawasiliano na koloni yao huko Uhindini kama wangetwaa Afrika Kusini. Baada ya miake kadhaa Waingereza walinyang'anya eneo hili rasmi mwaka 1806. Hali hii ilitambuliwa na Uholanzi 1815 kwenye Mkutano wa Vienna.

Koloni ya Rasi iliendelea chini ya Uingereza hadi 1910. Mwaka ule Muungano wa Afrika Kusini yaliundwa na rasi iliingia kama "Jimbo la Rasi".