Mpumalanga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mpumalanga
Mji Mkuu Nelspruit
’‘‘Mji Mkubwa’’’ Nelspruit
Waziri Mkuu Thabang Makwetla (ANC)
Eneo
Nafasi ya 8 kati ya majimbo ya Afrika Kusini
- Jumla 79 490 km²
Wakazi Nafasi ya 5 kati ya majimbo ya Afrika Kusini
- Jumla (2001) 3 122 994
- Msongamano wa watu / km² 39/km²
Lugha SiSwati (30.8%)
IsiZulu (26.4%)
IsiNdebele (12.1%)
Sepedi (10.8%)
Wakazi kimbari Waafrika Weusi(92.4%)
Wazungu (6.5%)
Chotara(0.2%)
Wenye asili ya Asia (0.2%)
Mahali pa Mpumalanga


Mpumalanga (kabla ya 2002 iliitwa Eastern Transvaal) ni moja kati ya majimbo 9 za Afrika Kusini. Kuna wakazi 3,364,000 (2001) kwenye eno la 79,512 km². Jimbo lilianzishwa mwaka 1994 kutokana na sehemu za jimbo la awali la Transvaal na maeneo ya bantustan KaNgwane, KwaNdebele na Lebowa. Mji mkuu ni Nelspruit.

Neno Mpumalanga limetokana katika lugha ya Kiswazi likimaanisha "mahali pa macheo".

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Mpumalanga imepakana na Eswatini na Msumbiji halafu na majimbo ya KwaZulu-Natal, Dola Huru, Gauteng na Limpopo. Hifadhi ya Kruger ambayo ni hifadhi ya wanyama mashuhuri imo jimboni.

Kuna kanda mbili za tambarare za juu penye usimbishaji kidogo na tambarare za duni penye mvua nyingi.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Kilimo[hariri | hariri chanzo]

Sehemu kubwa ya eneo hutumiwa kwa kilimo. Mazao ni pamoja na mahindi, ngano, ntama, alizeti, soya, karanga, miwa, mboga, kahawa, chai, pamba, tumbako, machungwa na matgunda mengine.

Misitu huvunwa hasa katika kaskazini penye kiwanda kikubwa cha karatasi cha Ngodwana.

Takriban 14% za eneo hutumiwa kwa mifugo hasa ng'ombe na kondoo.

Migodi[hariri | hariri chanzo]

Kati ya madini yanayochimbwa ni: dhahabu, platini, shabha, makaa mawe na mengi mengine.

Mpumalanga huzalisha 83% za makaa mawe ya Afrika Kusini.

Utalii[hariri | hariri chanzo]

Hifadhi ya Kruger ina eneo la 20,000 km² hutembelewa sana na watalii.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]


Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mpumalanga kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.