Nenda kwa yaliyomo

Limpopo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Limpopo, South Afrika
Limpopo
Eneo 123,900 km²
Wakazi(2001) 5,273,637
Lugha Sepedi, Venda, Tsonga
Wakazi kimbari Waafrika Weusi(97.3%)
Wazungu(2.4%)
Chotara(0.2%)
Wenye asili ya Asia (0.1%)
Mji Mkuu Polokwane
Waziri Mkuu Sello Moloto
(ANC)
Mahali pa Limpopo

Limpopo ni jimbo la kaskazini kabisa la Afrika Kusini. Mji mkuu ni Polokwane (zamani Pietersburg). Jimbo liliundwa kutokana na sehemu ya kaskazini ya jimbo la Transvaal ya awali na maeneo ya bantustan Venda na Lebowa.

Jina limetokana na mto Transvaal ambao ni mpaka wa jimbo na nchi jirani ya Zimbabwe.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Limpopo imepakana na Zimbabwe, Botswana na Msumbiji; halafu na majimbo ya Afrika Kusini ya Kaskazini-Magharibi, Gauteng na Mpumalanga.

Kuna milima mbalimbali hasa milima ya Waterberg na Drakensberg. Kaskazini kuna pori ya vichaka na maeneo ya magharibi tambarare za manyasi.

Wakazi na utamaduni

[hariri | hariri chanzo]

Kati ya wakazi amabo wamezidi milioni tano karibu nusu hutumia Kisotho cha Kaskazini. Vikundi vingine vikubwa ni Watsonga na Wavenda. Karibu wakazi wote ni Waafrika weusi, kuna Wazungu na chotara wachache.

Kilimo na madini ni uti wa mgongo wa uchumi. Utalii imeanza. Kuna migodi mikubwa ya shaba huko Messina na Phalaborwa.

Kilimo ni cha matunda katika kaskazini na ya mahindi, alizeti, pamba na karanga katika kusini.

Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Limpopo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.