Nenda kwa yaliyomo

Transvaal

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bendera ya Transvaal - "Vierkleur" (kwa maana ya rangi nne).
Ramani ya Transvaal

Transvaal ni eneo lililo kaskazini mwa Afrika Kusini.

Jina linamaanisha "ng'ambo ya mto Vaal".

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Hapo mwanzo, iliunda sehemu kubwa ya jamhuri huru ya Makaburu Kusini mwa Afrika. Baada ya Vita ya Uingereza dhidi ya Makaburu ya miaka 1899-1902 ikawa koloni la Kiingereza la Transvaal. Mwaka 1910 iliingia katika Muungano wa Afrika Kusini kama moja ya majimbo asilia manne. Pretoria ilikuwa moja ya miji mikuu ya Afrika Kusini ikiwa makao ya serikali hadi leo.

Baada ya mwisho wa mfumo wa ubaguzi wa apartheid majimbo ya Afrika ya Kusini yalipangwa upya na Transvaal ilikwisha kama jimbo la kisiasa. Maeneo yake yamekuwa majimbo mapya ya Gauteng, Limpopo na Mpumalanga na Jimbo la Kaskazini Magharibi. Ingawa haipo tena kama kitengo cha kiutawala, Transvaal bado ni neno la kijiografia linalotumiwa sana na lina maana yake ya kihistoria.

Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Transvaal kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.