Pretoria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru






Jiji la Pretoria

Bendera

Nembo
Jiji la Pretoria is located in Afrika Kusini
Jiji la Pretoria
Jiji la Pretoria

Mahali pa mji wa Pretoria katika Afrika Kusini

Majiranukta: 25°43′48″S 28°13′12″E / 25.73000°S 28.22000°E / -25.73000; 28.22000
Nchi Afrika Kusini
Majimbo Gauteng
Tovuti:  www.tshwane.gov.za
Kitovu cha mji wa Pretoria.
Ikulu ya Union House

Pretoria ni moja kati ya miji mikuu mitatu ya Afrika Kusini na makao makuu ya serikali. Miji mikuu mingine ni Cape Town kama makao ya Bunge na Bloemfontein kama makao ya Mahakama Kuu.

Pretoria iko kaskazini mwa jimbo la Gauteng katika bonde la milima ya Magalies kwenye kimo cha m. 1,370. Umbali na Johannesburg ni km. 56. Ni sehemu ya Jiji la Tshwane.

Jina la Pretoria ni la kumkumbusha jenerali wa Makaburu Andries Pretorius aliyeshinda Wazulu kwenye mapigano ya Mto wa Damu (Blood River) mwaka 1838. Kuna majadiliano kama jina la Pretoria libadilishwe pia kuwa "Tshwane".

Pamoja na ofisi za serikali kuna vyuo vikuu, hasa Chuo Kikuu cha Pretoria. Chuo Kikuu cha Afrika Kusini ni chuo kikubwa cha masomo kwa njia ya barua.

Pretoria ndio mji pekee wenye watu weupe (Wazungu) wengi kuliko mji wowote duniani nje ya Ulaya.

Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Pretoria kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.