Ndovu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Ndovu
Ndovu au Tembo
Ndovu au Tembo
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Proboscidea (Wanyama wenye mwiro)
Familia: Elephantidae (Wanyama walio na mnasaba na ndovu)
Ngazi za chini

Jenasi 2

Msambazo wa Ndovu wa Afrika (kijani) na Ndovu wa Asia (kahawia).
Msambazo wa Ndovu wa Afrika (kijani) na Ndovu wa Asia (kahawia).

Ndovu au tembo ni aina za wanyama wenye umbo kubwa kupita wanyamapori wote. Watoto wake wakizaliwa hufikia kg 100 na ndovu mzima huwa na uzito wa tani 2 hadi 5; kimo ni hadi m 4.

Kibiolojia ni mamalia. Sehemu ya pekee mwilini ni mwiro ambao hali halisi ni pua la tembo lililorefuka na kufanya kazi pia kama mkono wake yaani kwa kutumia mwiro ndovu hushika vitu na kufanya utafiti kwa kugusagusa.

Pembe-jino zake zinatafutwa sana kama mapambo na biashara ya pembe za ndovu imeshakuwa hatari kabisa kwa ndovu wote kwa sababu wanawindwa mno. Hivyo kwa mapatano ya kimataifa biahsara ya pembe hizi imepigwa marufuku.

Spishi[hariri | hariri chanzo]

Kwa jumla kuna spishi tatu za ndovu ambao wanafanana lakini hawazai pamoja. Ndovu-nyika ni mkubwa kuliko wengine.

Ndovu wa Asia ni mdogo wake lakini anazoea wanadamu kwa hiyo katika nchi kama Uhindi au Uthai hutumiwa kama mnyama wa kazi akibeba mizigo au watu. Zamani spishi hii ilitumiwa hata vitani. Kwa mfano jemadari Hanibal wa Karthago alishambulia Dola la Roma kwa msaada wa ndovu wa kijeshi waliovuka milima ya Alpi.

Ndovu-misitu alitazamiwa muda mrefu kama nususpishi ya Ndovu wa Afrika lakini wataalamu wamethebitisha ni spishi tofauti. Hufikia kimo cha mita 2 tu anaishi hasa katika misitu ya Kongo.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi ya Asia[hariri | hariri chanzo]

Chakula[hariri | hariri chanzo]

Ndovu hula manyasi na majani mengi. Kwa chakula hiki ambacho ni kigumu hutegemea meno yao. Meno haya pole yanachakaa kutokana na ugumu wa manyasi na baada ya kuharibu meno yote ndovu hufa.

Penye ndovu wengi mno wanaharibu miti. Wanapenda majani ya miti na hivyo wanavunja matawi ili wapate majani. Wakiweza wanaangusha pia mti wote kwa chakula hiki. Uharibifu huu ni tatizo katika mbguga za wanyama kadhaa ambako ndovu haziwzi kutoka nje kwa sababu nje wanavindwa.

Utangulizi[hariri | hariri chanzo]

Tembo ni mamalia wakubwa wa jenera ya familia ya ‘Elephantidae’; Elephas na ‘Loxodonta’. Kuna spishi watatu tu wa tembo wanaoishi mapaka leo. Tembo wa vichakani wa Africa (African Bushi Elephant), tembo wa misituni wa Africa (African Forest Elephant) na tembo wa Asia (Asian Elephant) Spishi wengine wote wa tembo wamepotea. Tembo ndiyo mamalia wan chi kavu wakubwa kuliko wote sasa. Tembo hubeba mamba kwa muda wa miezi 22, muda mrefu kuliko wanyama wote wa ardhini. Ndama wa tembo akizaliwa huwa na uzito wa kilogramu 120. Tembo huishi kwa kwa miaka 50-70, lakini tembo aliyevunja rekodi aliishi miaka 82.

Tembo mkubwa kupata kuishi alikuwa huko Angola na kupigwa risasi mnamo mwaka 1956. Tembo dume huyu alikuwa na uzito wa kg. 12,000, akiwa na kimo mpaka mabegani cha mita 4.2, mita moja zaidi kuliko tembo wa sasa wa Africa. Tembo wadogo, kama saizi ya ndama, au nguruwe mkubwa, waliishi zamani sana, huko visiwa vya Crete. Tembo wametokea sana kwenye tamaduni za dunia. Ni ishara/alama ya hekima huko Asia nani maarufu kwa uwezo wao wa kumbukumbu na akili, ambapo hufanikiwa kuwa wanakaribiana kuwa sawa na jamii ya binadamu wa kale. Mwanafalsafa Aristotle aliwahi kusema, “mnyama pori anayewapiku wengine wote kwa hekima na akili” Jina la tembo lina asili ya neno la kigiriki lenye maana ya ‘meno/pembe za ndovu. Tembo wakubwa hawana wanyama wanaowawinda ingawa samba huweza kuwashambulia ndama wa tembo na tembo wadhaifu. Japokuwa hutuishiwa sana na kuwa hatarini kutokana na mwingiliano na binadamu na ujangili. Kadiri ya sensa ya mwaka 2007, tembo wa Africa walikuwa kati ya 470,000 au 690,000. Tembo hulindwa duniani kote. Hii ni sambamba na maeneo maalumu ya kuwakamata, matumizi ya nyumbani na biashara kwenye mazao yake kama viel vipusa. Mataifa kadhaa yameripoti kupungua kwa tembo wao mpaka kufikia theluthi mbili, na hata wale walio kwenye maeneo tegefu nao wako hatarini kutoweka kutokana na kuongezeka kwa ujangili kwa zaidi ya asilimia 45% kupelekea hata takwimu za sasa kutokuwepo.

Tembo wa Africa[hariri | hariri chanzo]

Ndovu-nyika - Mikumi.

Tembo wa Jenasi ya ‘Loxodonta’, kwa ujumla hujulikana kama tembo wa Africa. Kwa sasa wanapatikana katika nchi 37. Tembo wa Africa hutofautishwa na tembo wa Asia kwa namna mbali mbali. Kwanza masikio yao ni makubwa sana na mwili wao ni mkubwa wenye mgongo uliopinda. Wote, dume na jike wa tembo wa Africa huwa na pembe za ndovu/vipusa kwa nje na miili yao huwa na nywele kidogo kuliko tembo wa Asia. Ndovu wa Africa hugawanywa kwenye makundi mawili kulingana na spishi zao, ndovu-nyika (Loxodonta africana africana) na ndovu-misitu (Loxodonta cyclotis). Tembo wa savanna wa Africa, ndiyo tembo mkubwa kuliko wote. Ndiyo mnyama wa ardhini aliye mkubwa kuliko wote, huku tembo dume akiwa na urefu wa mita 3.2 mpaka 4 mabegani na uzito wa kg. 3,500 mpaka 12,000. Tembo jike huwa mdogo kiasi huku wengi wakiishia urefu wa mita 3 tu.

Wengi wa tembo wa savanna wa Africa hupatikana katika nyika, mabwawani, na kwenye fukwe za ziwa. Hukaa sana kwenye kanda za savanna kusini mwa jangwa la Sahara. Spishi nyingine ya ndovu wa Africa ni ndovu-misitu (Loxodonta cyclotis), ambao ni wadogo na wa mviringo kiasi, pembe zao zikiwa fupi kiasi na zilizonyooka kuliko tembo wa savanna. Tembo wa misituni hufikia mpaka uzito wa kg. 4500 na husikia urefu wa mita 3. Mambo mengi hayafahamiki kuhusu tembo hawa ukivilinganisha na tembo wa savanna, kutokana na mazingira wanamoishi. Mara nyingi huishi katika misitu ya Africa, ile mizito nay a mvua, ya kati na magharibi mwa Africa. Japo mara chache husogea mipakanai mwa misitu yao, na kuzaliana na tembo wa savanna.

Tembo wa Asia[hariri | hariri chanzo]

Ndovu wa Asia

Tembo wa Asia ni mdogo kuliko tembo wa Africa ana masikio madogo, na kwa kawaida ni tembo dume tu ambao ndio huwa na pembe tu. Tembo wa Asia duniani, pia hufanika kama tembo wa India, hukaribia 60,000 walau mara moja ya kumi ya tembo wa Africa. Kwa ukaribu zaidi inakadiriwa kuwa tembo 38,000 mpaka 53,000 wapo misituni na 14,500-15,300 wanafungwa kwenye makazi ya watu nap engine 1000 hivi wametawanyika kwenye sehemu za kuonyeshea wanyama. Kupungua kwa tembo wa Asia, pengine ni kwa hali ya juu zaidi kuliko kwa tembo wa Africa kutokana na ujangili na uvamizi wa makazi ya tembo unaofanywa na binadamu.

Tembo wa savanna[hariri | hariri chanzo]

Hawa tembo wa Savanna (Elephas maximus sumatramus), wanapatikana tu hasa Sumatra, na ni wadogo kuliko India Elephant. Tembo hawa wana idadi takribani 2100 mpaka 3000. Wana rangi nyepesi ya kijivu kuliko tembo wengine wa Asia, na madoa ya pinki kwenye masikio yao. Tembo wa Sumatra huwa na urefu wa mita 1.7-2.6 mabegani mwao na uzito wao ni takribani kg. 3000

Mkonga[hariri | hariri chanzo]

Tembo

Tembo hutuma mkonga kwa kazi mbali mbali mojawapo kupukuta jicho lake. Mkonga ni muunganiko wa pua na mdomo wa juu, umenyooka na kuwa ogani muhimu kwa tembo. Tembo wa Africa wana vitu kama vidole viwili hivi mwishoni mwa mikongo yao, huku tembo wa Asia wakiwa na kimoja tu. Kulingana na wanabaiolojia, mkonga wa tembo unatakribani ya misuli 40,000 ndani yake, inayoifanya uwe na uwezo wa hata kuinua kipande kidogo cha kioo, vile vile kuwa na nguvu za hata kung’oa matawi ya misuli ndani ya mkonga wa tembo ni karibu ya 100,000 wanyama wengi wala majani hutumia meno yao chonge kurarua na kuchana majani. Hata hivyo, isipokuwa kwa wakiwa bado wadogo, tembo hutumia mikonga yao kuchuma chakula na kuweka kinywani mwao. Hula majani, matunda na matawi yake huangusha mti wote kabisa. Mkonga wa tembo hutumika pia kunywea maji. Tembo huvuta maji kupitia tundu za mkonga wake, mapaka lita kumi na nne kwa wakati mmoja, na kuyamimina kinywani mwake. Wakati mwingine hujimwagia maji mwilini kwa maana ya kuoga. Pia huweza kujipaka vumbi na tope, ambapo pindi hukauka huwa kama namna ya kujikinga na mwanga mkali wa jua. Wakati wa kuogelea, mkonga huwa kama neli yam zamia huwa nzuri kweli kweli. Mkonga pia hufanya kazi kubwa katika mahusiano ya jamii yake na wanyama wengine. Tembo husalimiana kwa kukutanisha na kuishikisha mkonga yao, sawia na binadamu anayosaliamana kwa kushikana mikono. Huitumia mikonga yao wakti wa kupishana, kupapasana na wenzi na pia mama anapoluwa anambembeleza mtoto. Pia pindi anapoinua mkonga wake humaanisha kusalimu amri. Tembo hujilinda wenyewe kutoka kwa wavamizi kwa kuwadaka na kuwabana.

Tembo pia hutegemea mkonga kwa ajili ya kunusa. Kwa kuinua mkonga hewani na kuyumbisha pande zote, na kama peviskopu, mkonga hutumika kutambua marafiki, maaduai na vyanzo vya chakula.

Pembe (au pembe-jino)[hariri | hariri chanzo]

Pembe za tembo ni kama meno ya pili ya chonge ya tembo hawa. Pembe hukua mfululizo, na kwa mwaka mmoja, huongezeka kwa sm 18 kwa tembo dume. Pembe hizi hutumika kuchimba kwa ajili ya maji, chumvi, miziz, kula magome ya miti, na kutaboa miti ya mibuyu kupata majimaji ya ndani. Pia hutumika kusafisha njia kwa kusogeza na kukata miti na matawi ya miti mikubwa. Pia hutumika kuweka alama kwenye miti kuonyesha mipaka ya hiamaya zao na mara kadhaa hutumika kama silaha.

Kama ilivyo kwa binadamu, wanapokuwa wanazoea kutumia sana mkono wa kulia ama kwa wengine wa kushoto, vivyo hivyo tembo nao huwa na ubobezi katika kutumia aidha pembe ya kushoto au kulia. Pembe inayotumika sana, huitwa penge kuu, kuwa fupi kidogo, na iliyolika kidogo kwenye ncha yake kutokana na matumizi. Tembo wote wa Africa, dume na jike huwa na pembe kubwa zinazoweza kufikia mita 3 kwa urefu na uzito wa kilo tisini. Tembo wa Asia huwa na pembe kwa dume pekee, lakini pembe zao huwa nyembamba na nyepesi, huku nzito kuliko zote kwao ilikuwa na uzito wa kg 39 Pembe kwa spishi zote huundwa kwa kalsiamu fosfeti, huku sehemu ya tishu hai ikiwa ni ndogo mno. Watu hutaka kupata pembe za tembo kwa wingi nao kumepelekea sana kuadimika kwa tembo hao kutokana na uwindaji wa tembo.

Kwa sababu ya ujangili wa ndovu ili kupata pembe zao aina za ndovu bila pembe zimetokea kwa mahali mbalibali, kaskazini kwa Msumbiji hasa. Ndovu hawa huitwa buda.

Meno[hariri | hariri chanzo]

Meno ya tembo ni tofauti sana nay ale ya mamalia wengine. Wakati wa maisha yao yote, huwa na jumla ya meno 28. haya hujumuisha meno change ba pili (hizi ndizo pembe), meno ya maziwa kabla ya pembe, magego madogo 12:3 kila upande wa taya, magego 12:3 kila upande wa taya.

Upande wa taya[hariri | hariri chanzo]

Tofauti na mamalia wengine ambao meno ya kitoto huanza na kupisha meno ya ukubwani ya moja kwa moja, tembo huwa na mzunguko wa meno kwa maisha yao yote. Pembe zao hutanguliwa na meno change mawili ambayo huondoka baada ya mwaka mmoja na pembe kuchomoza. Magego hubadilishwa walau mara tano katika maisha ya tembo. Meno hayatoki kutaka kwenye fidhi wima kama kwa binadamu isipokuwa, kutoka kwa ulalo, kama mkanda wa kusukumia mashine. Meno mapya hukua nyuma ya kinywa na kuyasukuma meno ya zamani nje. Tembo wanapozeeka sana, ile seti ya mwisho ya meno huisha na kuwa laini hata kushindwa tena kula na kutafuana na kutegemea tu chakula laini tu. Tembo hao wazee hutumia muda wao wa siku za mwisho kwenye maeneo wazi ambako wanaweza kula nyasi laini. Kwa bahati mbaya, meno yao ya mwisho yanapodondoka, tembo hao hushindwa kula na hufa kwa njaa. Isingekuwa kuisha kwa meno, tembo wangekuwa na uwezo wa kuishi kwa muda mrefu sana. Kwa sababu sasa makazi ya tembo yanazidi kuvamiwa na kuwa madogo mno, tembo wazee hukosa sehemu nzuri za kujipatia nyasi laini na hivyo hufa mapema kwa njaa.

Ngozi[hariri | hariri chanzo]

Tembo wana ngozi pana sana kwenye asilimia kubwa ya msuli wao na hukaribia sentimeta 2.5 kwa upana. Japo ngozi kwenye mdogo na sikioni ina upana wa karatasi tu. Ngozi ya tembo wa Asia huwa na nywele kiasi, hasa wakati wa utoto na kupungua wakati wanapoendelea kukua; huku tembo wa Africa wakiwa hawana nywele kabisa.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Crystal Clear app babelfish.png Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ndovu kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
Wa mifupa ya tembo na mtu.

Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.