Uharibifu wa mazingira
Uharibifu wa mazingira ni uzoreteshaji wa mazingira kwa njia ya kupunguza rasilimali kama vile hewa, maji na udongo na kupotea kwa wanyamapori. Uharibifu wa mazingira ni wa aina nyingi. Wakati ni makazi asili yanaharibiwa au maliasili kutumiwa vibaya, tunasema kuwa mazingira yanaharibiwa.
Uharibifu wa mazingira ni moja ya vitisho kumi vilivyoonywa na jopo la juu la vitisho vikuu la Umoja wa Mataifa. Shirika la raslimali ulimwenguni, Umoja wa Mataifa wa Mpango wa Mazingira, Umoja wa Mataifa wa Maendeleo na Benki ya Dunia zimetoa ripoti kwa umma kuhusu afya na mazingira duniani tarehe 1 Mei 1998.
Mabadiliko ya mazingira na afya ya binadamu, sehemu maalum katika ripoti hiyo inaeleza jinsi magonjwa yana uwezo wa kuzuiwa na vifo vya mapema bado huzidi kuongezeka kwa idadi kubwa. Ikiwa kuna marekebisho makubwa katika afya ya binadamu mamilioni afya ya binadamu, mamilioni ya watu watakuwa wangeishi kwa muda mrefu,na maisha yenye afya nzuri kuliko awali. Katika maeneo maskini katika dunia inakadiriwa kuwa mmoja katika watoto watano hawataishi kuona siku yao ya kuzaliwa ya tano, hasa kwa sababu ya magonjwa yanayohusiana na mazingira. Watoto Milioni kumi na moja duniani kote hufa kila mwaka, sawa na wakazi wa Norway na Uswisi, wakiunganishwa na hasa kutokana na malaria, shida za kupumua au kuhara - magonjwa ambayo yanaweza kukingwa.
Madhara ya uharibifu wa mazingira
[hariri | hariri chanzo]Hili suala huleta madhara makubwa hasa kwa jamii maana huweza kusababisha vifo na hivyo nguvukazi ya taifa hupungua ambapo hukwamisha maendeleo ya taifa na kuleta changamoto kubwa kwa jamii au taifa kwa ujumla.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Ikolojia ya ongezeko la Magonjwa , ukuaji wa Idadi ya Watu na uharibifu wa mazingira. Archived 12 Novemba 2016 at the Wayback Machine.
- Matokeo ya Shirika la Marekani la Wanajiografia la Mabadiliko ya Kimazingira Katika Kalahari :Utafiti wa Uharibifu wa Ardhi Katika Mazingira Yenye ardhi Kavu
- Tishio fupi la Umma : Uharibifu wa mazingira
- Focus: uharibifu wa mazingira ni vitisho kuchangia afya duniani kote Archived 3 Machi 2016 at the Wayback Machine.
- Uharibifu wa mazingira kwa vifaa vya nuklia . Archived 11 Novemba 2016 at the Wayback Machine.
- Kiashiria cha Uharibifu wa mazingira na Jha & Murthy (kwa nchi 174) Archived 28 Septemba 2007 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Uharibifu wa mazingira kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |