Nenda kwa yaliyomo

Jani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Majani)
Majani yenye umbo la sindano
Muundo wa jani

Jani ni ogani ya mimea na kazi yake ya msingi ni usanisinuru na upumuaji (badiliko la gesi). Kwa hiyo ni sehemu ya mmea iliyopo juu ya ardhi.

Umbo lake mara nyingi ni bapa na nyembamba. Ubapa unaisaidia kuwa na uso mkubwa kwa kupokea nuru nyingi iwezekanavyo, na wembamba unasaidia nuru kufikia seli ambako inatumiwa na vyembe vya viwiti kuendesha usanisinuru.

Umbo tofauti ni kama sindano. Maumbo ya jani kama sindano au miiba yanatokana na mazingira ambayo ni yabisi, ama kwa miezi kadhaa au kwa muda mrefu zaidi.

Hili ni pia umbo la majani ya kudumu ya miti inayoweza kustawi katika mazingira yenye jalidi kama vile misunobari.

Muundo wa jani

[hariri | hariri chanzo]
  • Jani hufunikwa na ngozi ya nje ambayo ni ganda jembamba sana la nta. Chini yake ni epidemisi au ngozi ya ndani. Katikati ya maganda haya ya nje kuna seli za kati (mesophyll). Kuna aina mbili za seli hizi:
  • Seli safu za kati zenye umbo la mcheduara ndefu kidogo zikipangwa kwa safu. Ndani ya seli hizi kuna idadi kubwa ya viwiti vinavyopokea nuru, viko moja kwa moja chini ya epidemisi upande wa juu ya jani na kuelekea nuru
  • Seli sifongi za kati ziko chini ya seli safu, hazipangwi ipasavyo na kuna viwiti vichache tu. Vina nafasi kati yake zinazounganishwa na vinyweleo.
  • Ngozi ya jani ya chini huwa na vinyweleo, kila kinyweleo huwa na seli linzi kando yake. Hapo ni nafasi ya jani "kupumua" yaani kuingiza dioksidi kabonia na kutoa oksijeni.
  • Ndani ya jani lote kuna vitita neli vyenye kazi ya mishipa damu na mifupa kwa pamoja. Kitita neli ni kama fungo la "mabomba" yanayoundwa kwa seli za pekee zinazosafirisha virutubisho ndani ya jani hadi tawi au shina na mizizi.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jani kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.