Jalidi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Jalidi ni hali ya baridi ambako halijoto inafikia chini ya kiwango cha sentigredi 0. Hii ni kiwango ambako maji yanaanza kuganda kuwa barafu.

Jalidi kama halijoto inaathiri viumbehai na mimea kwa sababu huwa na maji katika miili yao. Mimea inakufa katika hali ya jalidi kama maji ndani ya seli zao inaganda; maji ikiganda inapanua mjao wake hivyo kupasua seli. Mimea hii au sehemu zao zilizokufa huwa nyeusi na hali hii hutiwa jalidi pia (Kiing.: black frost).

Mimea ya nchi ambako jalidi ni hali ya kawaida wakati wa majira ya baridi ina uwezo wa kukauka kabla ya majira ya jalidi kuanza. Katika mazingira ya joto mimea hufa mara nyingi kama baridi huwa kali.

Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jalidi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.