Tundra

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Arctic tundra on Wrangel Island, Russia

Tundra ni eneo ambako miti haiwezi kustawi kutokana na halijoto duni na kipindi kifupi cha kuota kwa majani. Mara nyingi ardhi ya maeneo haya iko katika hali ya sakitu ya kudumu yaani halijoto ya ardhi chini ya kina cha sentimita 30-200 ina halijoto chini ya sentigredi 0°C muda wote hata katika wakati wa "joto" katika maeneo haya.

Kuna aina tatu za tundra:

Uoto wa mimea katika maeneo ya tundra ni hasa majani, kumvumvani na kuvu. Kama miti iko inatokea kwa umbo la vichaka vidogo. Mpaka kati ya maeneo ya tundra na maeneo ya misti hujulikana kama "mstari wa miti".

Tabianchi katika maeneo ya tundra ni baridi kali na halijoto kidogo juu ya 0°C wakati wa wiki au miezi michache ya majira ya joto ilhali joto halitoshi kuyeyusha ardhi iliyoganda isipokuwa kwenye sentimita za juu za ardhi.


[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. English through Science (2010). Blue Planet. McGrawHill.