Epidemisi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Epidemisi ni sehemu ya juu ya ngozi, na sehemu ya ndani huitwa demisi. Epidemisi ni neno lenye asili ya Kigiriki linalomaanisha "juu ya demisi".

Yenyewe huzuia maambukizi kutoka katika mazingira na vijidudu na inasimamia kiasi cha maji kinachotolewa kutoka mwilini kupitia jasho.

Sehemu ya nje kabisa ya ngozi ya juu inajumuisha tabaka la seli bapa, ambazo hujumuisha seli safuwima pangwa (perpendicularly).

Epidemisi ina unene wa milimita 0.03 hadi 0.05 lakini imaweza kufikia unene wa milimita kadhaa chini ya miguu na kwenye makofi ya mikono. Haifikiwi na mishipa ya damu. Hii ngozi ya nje hasa ina kazi ya kukinga mwili.

Ndani yake kuna kanda mbalimbali; sehemu ya chini ni kanda la kizazi ambako seli mpya zinazalishwa; jinsi zinavyosukumwa kuelekea nje zinakauka na mwishoni zifikia nje kabisa zinatoka kama mba.

Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Epidemisi kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.