Patrice Lumumba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha halisi ya Patrice E. Lumumba.

Patrice Lumumba (2 Julai 192517 Januari 1961) alikuwa mwanasiasa na kiongozi wa uhuru wa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mwaka wa 1958 alikuwa miongoni mwa waanzishaji wa Chama cha Taifa la Kongo (kwa Kifaransa: Mouvement National Congolais).

Mwaka wa 1960 alipata kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya kuongoza harakati za kugombea uhuru toka kwa utawala wa kikoloni wa Wabelgiji.

Baada ya miezi miwili tu ya kuwa Waziri Mkuu, Lumumba alipinduliwa na baadaye kutiwa ndani kabla ya kuuawa katika mazingira ya kutatanisha katika eneo la Katanga upande wa kusini wa Kongo.

Hadi kufikia uwaziri mkuu[hariri | hariri chanzo]

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Patrice Lumumba alizaliwa katika familia ya Watetela, wazazi wake walikuwa François Tolenga Otetshima, na Julienne Wamato Lomendja, ambao walikuwa wafugaji katika eneo la Katakokombe kwenye Mkoa wa Kasai.[1] Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Élias Okit'Asombo alilobadilisha baadaye.[2] na asombó ('cursed or bewitched people who will die quickly').[3] Alikuwa na kaka watatu ambao ni Charles Lokolonga, Émile Kalema, and Louis Onema Pene Lumumba.[1]Alilelewa katika makuzi ya Kikatoliki, alisoma katika shule ya msingi ya Waprotestanti, halafu katika shule ambayo iliyomilikiwa na wamisionari wa Kanisa Katoliki, na baadaye alipata mafunzo katika chuo kimoja cha serikali, alijishindia kozi mbalimbali na kisha kuajiriwa, alipata kazi katika mji wa Stanleyville ambao kwa sasa unajulikana kwa jina la Kisangani ambapo alifanya kazi kama karani wa posta.

Baadaye alihamia Léopoldville ambao kwa sasa unajulikana kwa jina la Kinshasa alipofanya kazi ya uuzaji wa bia kwa wasafiri. Mnamo mwaka 1951 alimuoa Pauline Opangu. Mwaka 1955 Lumumba alijiunga na Cercles des évolués ambazo zilikuwa klabu za Waafrika wenye elimu ya kibelgiji na kutazamwa kuwa "wameendelea" mjini Stanleyville na baadaye alijiunga na chama cha Liberal Party of Belgium, ambapo alifanya kazi ya uhariri na usambazaji wa kijarida cha Chama cha Kiliberali cha Ubeljiji. Baadaye alifanya ziara ya mafunzo ya wiki tatu nchini Ubeljiji, mwaka 1956 alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la ubadhirifu na kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kifungo cha nje na, kisha wakili wa Kibelgiji kuthibitisha kwamba Lumumba amesharejesha zile fedha, aliachiliwa huru mapema mwaka uleule.

Baada ya kuachiliwa kwake alisaidiwa na kuanzisha chama cha w:Mouvement national congolais (MNC). Mwaka 1958, alichaguliwa kuwa Rais wa chama hicho. Mnamo Desemba 1958 Lumumba na wenzake walikiwakilisha chama chao katika mkutano wa Baraza la watu wote wa Afrika mjini Accra, Ghana, katika mkutano huo wa Desemba wa muungano wa Afrika uliokuwa chini ya Rais wa Ghana Kwame Nkrumah, Lumumba ambaye alionekana kuongea lugha nyingi, zikiwemo za Kitetela, Kifaransa, Lingala, Kiswahili, na Kiluba, alijitambulisha kwa imani yake kwa bara la Afrika. .[1]

Uongozi wa MNC[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwezi wa Oktoba, mwaka 1959, Lumumba, kama kiongozi wa chama cha MNC, alikamatwa kwa kosa la kuchochea vurugu za kupinga serikali ya kikoloni katika mji wa Stanleyville ambapo watu takriban 30 waliuawa na yeye alihukumiwa kwenda jela kwa muda wa miezi sita. Mnamo tarehe 18 Januari 1960 ambayo ilikuwa siku ya majaribio na hapohapo katika siku ya kwanza ya mkutano wa kuzungumzia hatma ya nchi ya Kongo itakumbukwa kwamba, licha ya Lumumba kuwa jela katika kipindi hicho, chama chake cha MNC kilifanikiwa kuwashawishi wananchi kwenye uchaguzi uliofanyika mwezi Desemba na kushinda katika jamhuri ya Kongo. Kutokana na nguvu ya umma iliyokuwa ikifanywa na wananchi wa Kongo dhidi ya kuachiliwa kwa Lumumba kutoka kila kona, aliachiliwa na kuruhusiwa kuhudhuria katika mkutano wa Brussels. Mkutano huo ulifikia kilele tarehe 27 June 1960 kwa azimio la uhuru wa nchi ya Kongo na kupanga uchaguzi kwa mwaka huohuo wa 1960 (Uchaguzi Mkuu wa Kongo 11–25 Mei 1960.

Lumumba na chama chake cha MNC walipata ushindi uliowawezesha kuunda serikali kwa tangazo la tarehe 23 June 1960 na Patrice Lumumba anapata cheo cha uwaziri mkuu akiwa na umri wa miaka 34 na Joseph Kasa-Vubu akiwa ndie Rais wake wa kwanza. Kwa mujibu wa katiba ya Congo mnamo tarehe 24 June serikali ilipitisha kura ya kijasiri ambayo iliamuliwa na baraza la maseneta kwamba tarehe 24 iwe ni siku ya ya kuadhimisha uhuru wa Congo.

Maadhimisho ya uhuru wa Congo kwa mara ya kwanza yalifanyika mnamo tarehe 30 June 1960 ambapo maadhimisho hayo yalihudhuriwa pia na Mfalme Baudouin wa Ubelgiji pamoja na vyombo mbalimbali vya habari kutoka nchi za nje. Lumumba alitoa hotuba yake kama Waziri mkuu katika nchi huru japo yeye alikuwa ameenguliwa katika ratiba ya shughuli hiyo.[4] Mfalme wa Ubeljiji alihutubia kwa kutukuza utawala wa kikoloni, huku akilingania fikra za mjomba wake ambaye alikuwa mfalme wa Ubelgiji akiitwa Leopold II wa Ubelgiji bila kutaja maangamizi ya Dola huru la Kongo. Mfalme aliendelea kutoa masharti, "aliwataka kutokufanya mabadiliko yoyote mpaka wao watakapoona kwamba wanaweza kufanya vyema, na kwamba wataendelea kutoa ushauri. "[5] Lumumba aliufahamisha umma kwamba uhuru uliotolewa na Wabeljiji haukuja hivihivi:[5]

kwa uhuru huu wa Congo hata kama tunasherehekea leo na Wabeljiji, nchi rafiki ambayo tupo sawa kwa sawa, hakuna Mkongo hata mmoja ambaye atasahau kwamba vita waliyipigana hatimaye wakashinda wamaeshinda, kwa mapambano yaliyokuwa yakiendelea, mapambano ambayo watu tulijitoa ambayo kwayo watu walikuwa tayari kwa lolote hata kumwaga damu, kwa namna kwa hakika yalikuwa mapambano matukufu na yalikuwa na mwelekeo wa kukomesha utumwa ambao ulikuwa ukiendeshwa dhidi yetu kwa nguvu.[5]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 Kanyarwunga, Jean I N (2006). République démocratique du Congo : Les générations condamnées : Déliquescence d'une société précapitaliste. Paris: Publibook. p. 76. ISBN 9782748333435. 
  2. Hagendorens, MGR J (1975). Kamusi ya -Kifaransa. Bandundu: Ceeba Publications. pp. 275–76. 
  3. Hagendorens, MGR J (1975). Kamusi ya –Kifaransa. Bandundu: Ceeba Publications. pp. 309, 371. 
  4. hotuba ya siku ya maadhimisho ya uhuru. Iliwekwa mnamo 15 July 2006.
  5. 5.0 5.1 5.2 Kamalu, Chukwunyere. Kitabu cha historia ya wafrica –Africa nyeusi kutoka katika uharisia wa mwanadamu.ukurasa wa 115

Filamu[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Patrice Lumumba kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.