Brussels

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru







Bruxelles/Brussel
Brussels

Bendera
Majiranukta: 50°51′N 4°21′E / 50.850°N 4.350°E / 50.850; 4.350
Nchi Ubelgiji
Jimbo Brussels
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 1,080,790
Tovuti:  www.brucity.be
Nyumba ya baraza la jiji (Hôtel de ville)

Brussels (Kifaransa: Bruxelles, Kiholanzi: Brussel, Kijerumani: Brüssel) ni mji mkuu wa Ubelgiji na pia makao makuu ya ofisi za Umoja wa Ulaya.

Kisheria jina la Brussels linataja mambo mbalimbali:

- mji wa Brussels wenye wakazi 142,000 kwenye eneo la kilometa za mraba 32.

- Jimbo la Brussels ambamo ndipo ulipo mji wa Brussels pamoja na miji 18 mingine inayojitawala. Sehemu hizi zote ni hali halisi kama mji mmoja mkubwa lakini kisheria kila sehemu bado ina hali yake ya pekee. Jimbo lina wakazi milioni moja. Cheo cha mji mkuu kinamaanisha jimbo lote si mji pekee yake.

Mji umejulikana tangu mwaka 966 BK lakini kuna uwezekano ya kwamba umri wake ni mkubwa. Katika karne ya 15 BK ulikuwa mji mkuu wa utemi wa Brabant ukitajirika kutokana na karakana zake za nguo na biashara yake. Baadaye Brussels pamoja na Ubelgiji ilikuwa chini ya watawala wa nje kwanza Hispania halafu Uholanzi. Mapinduzi wa 1830 yalileta uhuru na Brussels ikawa mji mkuu wa taifa jipya katika Ulaya. Katika karne ya 19 mji uilikua sana katika mapinduzi ya viwandani.

Tangu 1958 Brussels imekuwa mji mkuu wa Ulaya kwa sababu imeteuliwa kuwa makao makuu ya ofisi za Umoja wa Ulaya - wakati ule mtangulizi wake Jumuiya ya Kiuchumi ya Ulaya. 1967 makao makuu ya NATO yalifuata ikahamia baada ya fitina kati ya Marekani na Ufaransa.

Kati ya majengo maarufu sana za Brussels ni Atomium iliyosimamishwa wakati wa Maonyesho ya Dunia 1958.

Makala hii kuhusu maeneo ya Ubelgiji bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Brussels kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.