Nelson Mandela

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Tuzo Nobel.png
Nelson Mandela

Nelson Rolihlahla Mandela (18 Julai, 1918 - 5 Desemba, 2013) alikuwa rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia nchini Afrika Kusini.

Alikuwa mwanasheria na mwanachama wa chama cha ANC aliyepinga siasa ya ubaguzi wa rangi (Apartheid) katika Afrika Kusini.

Mandela alihukumiwa kifungo cha maisha kwa miaka 27 kutokana na harakati zake za kuupinga ubaguzi wa rangi. Alifungwa katika kisiwa cha Robben.

Baada ya kuachiliwa huru mwaka 1990 alianzisha sera ya maridhiano au sera ya amani baina yake na watu weupe nchini Afrika Kusini jambo ambalo watu wengi hawakulitegemea.

Mwaka wa 1993, pamoja na Frederik Willem de Klerk alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani ambayo ni tuzo nadra sana kutolewa duniani.

Aliyekuwa mke maarufu wa Nelson Mandela, Winnie Madikizela, baada ya kutengana naye aliwahi kuwa mke wa rais wa Msumbiji, Samora Machel.


Administradors.png Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nelson Mandela kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.