Harambee

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Harambee ni neno ambalo lilitungwa na hayati Mzee Jomo Kenyatta (rais wa kwanza wa Jamhuri ya Kenya) ili kuwapa motisha wafanyakazi na hasa wale wanaofanya kazi nzitonzito.

Harambee hutoka kwa neno la Kihindi, Har Ambee, ambalo ni sifa kwa miungu wa kihindi wawape nguvu na uwezo wa kufanya kazi.

Neno hili lilisikika sana wakati wahindi walitumiwa kama vibarua wa kutengeneza reli kati ya Nairobi na Mombasa.

Kisha likatoholewa na mwishowe likaja kujulikana kumaanisha "tuvute pamoja"

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Harambee kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.