Nenda kwa yaliyomo

Malcolm X

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Malcolm X
Malcolm X in March 1964
Malcolm X mnamo Machi 1964
AmezaliwaMalcolm Little
(1925-05-19)Mei 19, 1925
AmekufaFebruari 21, 1965 (umri 39)
Manhattan, New York
Sababu ya kifoKauawa kwa risasi
Majina mengineel-Hajj Malik el-Shabazz
(الحاجّ مالك الشباز)
Kazi yakeMinister, activist
AsasiNation of Islam,
Muslim Mosque, Inc.,
Organization of Afro-American Unity
NdoaBetty Shabazz (m. 1958–present) «start: (1958)»"Marriage: Betty Shabazz to Malcolm X" Location: (linkback://sw.wikipedia.org/wiki/Malcolm_X)
WatotoAttallah Shabazz
Qubilah Shabazz
Ilyasah Shabazz
Gamilah Lumumba Shabazz
Malikah Shabazz
Malaak Shabazz
WazaziEarl Little
Louise Helen Norton Little
Saini[[File:{{{signature}}}|150px|alt=]]

Malcolm X (jina lake la awali lilikuwa Malcolm Stuart Little; baadaye alifahamika kama Hajj Malik; 19 Mei 1925 - 21 Februari 1965) alikuwa mwanaharakati wa Haki za binadamu za Waafrika-Waamerika na haki za kiraia kwa jumla

Malcolm katika kipindi chote cha ukuaji wake aliishi kwa ndugu baada ya kifo cha baba yake na mama yake kwenda kuishi hospitali kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.

Alijihusisha na shughuli za uhalifu katika maisha yake ya awali na kuhukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani mwaka 1946 kwa makosa ya uvunjaji na wizi. Akiwa gerezani alijiunga na Taifa la Uislamu na hapo ndipo alipojipachika jina Malcolm X akimaanisha jina lake la Kiafrika ambalo hakupatiwa kutokana na athari za utumwa. Baada ya kuachiwa toka gerezani mwaka wa 1952 kwa kuonesha tabia njema, kwa haraka sana alipata kuwa mtu mashuhuri ndani ya Taifa la Uislamu.

Vitendo[hariri | hariri chanzo]

Mara ya kwanza, matendo na mazungumzo ya Malcolm X yalikuwa yanaongozwa na imani na mafundisho ya Taifa la Uislamu. Alifundisha kwamba watu wote weupe walikuwa wabaya.

Mara alipojifunza kwamba kiongozi wa Taifa la Uislamu alikuwa katika mahusiano na wanawake wengi, aliacha kikundi akabadili dini yake kwa Uislamu wa Sunni. Aliendelea safari ili kuona mji mtakatifu wa Kiislamu wa Makka huko Saudi Arabia. Kwa wakati huu, mawazo yake ya watu weupe yalikuwa bora, akaanza kuamini kwamba Wazungu pia wanaweza kuwa watu wazuri. Malcolm X aliamini kuwa watu weusi wanapaswa kupigana kwa ajili ya haki zao za kiraia kwa njia yoyote waliyoweza, hata kama walipaswa kuleta vurugu. Pia alifikiri kuwa watu weusi wanapaswa kusaidiana kwa kununua vitu katika maduka yaliyomilikiwa na watu weusi. Alikuwa muhimu kwa harakati za haki za kiraia.

Kifo[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 19 Februari 1965, Malcolm X alimwambia mwanahabari Gordon Parks kwamba Taifa la Uislamu lilikuwa likijaribu kumuua. Februari 21, 1965, alikuwa akijiandaa kuhutubia OAAU katika mitaa ya Manhattan katika jengo la Audubon Ballroom.

Alipigwa risasi ya kifua na bunduki aina ya shotgun. Alitangazwa kufariki punde baada ya kufikishwa katika hospitali ya Columbia Presbyterian Hospital. Uchunguzi ulionesha alipigwa risasi 21 katika maeneo ya kifua bega la kushoto, mikono na miguu.

Wauaji watatu baadaye walitambulika kama wanakikundi wa Taifa la uislamu ambao ni William 25X, aliyejulikana pia kama William Bradley, ambaye alimpiga risasi na Leon Davis pamoja na Thomas Hayer

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Alikuwa na watoto sita na Betty Shabazz. Alikuwa na wajukuu sita. Malcolm Shabazz ambaye alikuwa mjukuu wa kwanza wa kiume wa Malcolm X aliuawa Mei 9 2013. Yeye pia ana wajukuu wawili.

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Malcolm X kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.