Ziara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ziara (kwa Kiingereza: trip au travel) ni nomino inayoashiria kutembea au kuzuru mahala fulani. Inawezekana ukafanya ziara pahala ambapo ni ng'ambo na nchi yako au hata ndani ya nchi yako.

Ziara yaweza kufanywa na mtu mmoja au hata kundi la watu. Ziara hufanywa na familia sanasana wakati wa likizo wakati watoto wako nyumbani na wazazi wamepewa ruhusa ya kupumzika nyumbani.

Ziara kwa ndege

Yaweza kufanyika kwa mbinu tofauti za usafiri kama miguu, baiskeli, gari, garimoshi, meli au hata ndege.

Madhumuni ya ziara[hariri | hariri chanzo]

Ziara hufanyika kwa sababu tofauti. Waweza ukazuru mahala kwa sababu hizi:

  • Kujifurahisha
  • Kupumzisha akili na mwili
  • Kuona mageni
  • Kujua jamii nyingine na kukagua wanavyofanya mambo
  • Kuchukua wakati kutengeneza uhusiano na watu wengine wa mahala tofauti
  • Usafiri kwa gari moshi

Historia ya ziara[hariri | hariri chanzo]

Zamani ziara zilifanywa kwa minajili ya kutafuta riziki au kwa sababu ya usalama iwapo ulipo hapana chakula cha kutosheleza jamii yako au kuna usalama duni. Ziara pia zilifanywa kwa sababu ya biashara za kuchuuza watumwa na bidhaa kama chumvi na mifugo.

Kwa leo hii, ziara hufanywa kwa madhumuni haya lakini watu wamekuwa wakifanya ziara sanasana kwa madhumuni ya raha. Kwa mfano, Wazungu hutembelea Afrika ili waweze kuona wanyamapori na pia kuangalia jamii za Kiafrika. Watu hutembea nchini Israel ili waweze kusali na kufuata kumbukumbu za Biblia. Watu hutembelea jijini York, Uingereza waweze kuona York Minster na The National Railway Museum. Watu hutembea jijini Las Vegas waweze kucheza kamari na kujitosa katika anasa.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ziara kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.