Kamari

Kamari (kutoka Kiarabu) ni mchezo wa bahati nasibu unaohusisha pesa au kitu kingine chenye thamani kama tuzo kwa mshindi. Tuzo hilo la kubahatisha ndio lengo la mchezo.
Sheria za nchi zinatofautiana kuhusu uhalali wake.[1][2][3]
Hata maadili ya dini yanatofautiana. Kwa mfano dini ya Uislamu inakataza kabisa moja kwa moja uchezaji wa kamari [4][5][6][7][8]
Tatizo mojawapo kubwa ni kwamba wanaoshiriki michezo hiyo wanahitaji au kutamani sana utajiri, hivyo wakishindwa wanaweza kushawishika kucheza tena na tena hadi kufilisika. Baadhi ya wachezaji wa michezo hii hufikia hata kupata matatizo au ugonjwa wa akili. Kuna tiba za aina mbalimbali za kuwasaidia watu wanaoshindwa kuwa na uamuzi wa kuacha michezo hii kutokana na uraibu.
Michezo ya kamari imekuwa biashara kubwa kimataifa, ikiwa na bajeti ya dola bilioni 335 mwaka 2009.[9] Umaarufu wa michezo kama vile soka na teknolojia mpya imefanya michezo hii kupata umaarufu wa kasi kubwa duniani.[10]
Tanbihi[hariri | hariri chanzo]
- ↑ Gambling and the Law®.
- ↑ Humphrey, Chuck. Gambling Law US. Gambling Law US. Iliwekwa mnamo 2012-09-22.
- ↑ UK Gambling Commission. Gamblingcommission.gov.uk. Iliwekwa mnamo 2012-09-22.
- ↑ Bose, M. L. (1998). Social And Cultural History Of Ancient India (revised & Enlarged Edition). Concept Publishing Company, 179. ISBN 978-81-7022-598-0.
- ↑ Berel Wein. Gambling. torah.org. Jalada kutoka ya awali juu ya 2010-06-16. Iliwekwa mnamo 20 July 2010.
- ↑ Kucharek, Rev. Cass (1974). To settle your conscience a layman's guide to Catholic moral theology.. Our Sunday Visitor. ISBN 0-87973-877-4.
- ↑ Blaise Pascal: Mathematician, Physicist and Thinker about God, [[Donald Adamson]] (1995). Jalada kutoka ya awali juu ya 2015-09-11. Iliwekwa mnamo 2021-12-30.
- ↑ International Association of Gaming Regulators: Members. Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-11-16. Iliwekwa mnamo 2015-08-20.
- ↑ "You bet", The Economist, 8 July 2010.
- ↑ Programu ya Playtech
Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]
- Gambling sites katika Open Directory Project
- Center for Gaming Research - at University of Nevada, Las Vegas
- Institute for the Study of Gambling and Commercial Gaming at the University of Nevada, Reno
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kamari kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |