Bilioni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchoro unaoonyesha bilioni kupitia michemraba A, B, C na D, ambapo A inaingia katika B, B katika C na C katika D.

Bilioni (kutoka Kiingereza "billion"[1][2]) ni namba ambayo inamaanisha milioni elfu moja na kuandikwa 1,000,000,000.

Inafuata 999,999,999 na kufuatwa na 1,000,000,001.

Inaweza kuandikwa pia kifupi 1 × 109.

Kiambishi awali giga kinatumika pia kumaanisha mara 1,000,000,000, ingawa katika lugha nyingine nyingi neno linalofanana na "bilioni" linamaanisha milioni milioni (1,000,000,000,000).

Matumizi tofauti[hariri | hariri chanzo]

Katika Kiingereza cha Uingereza hadi mwaka 1964 neno "milliard" lilikuwa kawaida kwa namba inayoitwa sasa "bilioni". "Bilioni" ilikuwa kawaida cha Kiingereza cha Marekani tu, lakini ilingia polepole pia katika matumizi ya Kiingereza cha kimataifa.

Mwaka 1974 serikali ya Uingereza ikaamua kutumia umbo hilo.[3] [4]

Kwa Kiingereza mifumo hii miwili kwa kutaja namba kubwa sana huitwa "short scale" (Kimarekani) na "long scale" (Kiingereza cha zamani).

Nchi nyingine, hasa za Ulaya, Afrika na Amerika ya Kilatini zimeendelea kutumia "long scale" kwa lugha kama Kifaransa, Kijerumani au Kihispania. Kwa hiyo katika nchi hizo 1,000,000,000 huitwa kwa neno kama "miliardi" na bilioni ni namba ya "milioni x milioni".

Tofauti inaweza kuleta mara nyingi makosa kama matini inatafsiriwa au kama kitabu cha kale kutoka Kiingereza hutumiwa.

Matumizi ya mifumo ya "short scale" na "long scale" duniani
     "Short scale", 1,000,000,000 au 109 inaitwa bilioni      Long scale, 1,000,000,000 au 109 inaitwa miliardi      Mifumo yote miwili kandokando      Mifumo tofauti

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bilioni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.