Mchemraba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchemraba huwa na pande 6 zenye urefu na upana sawa
Mchemraba ukizunguka

Mchemraba ni gimba lenye pande sita mraba. Ni aina ya pekee ya mchestatili.

Mjao[hariri | hariri chanzo]

  • Mjao wa mchemraba unapatikana kwa kuzidisha urefu kwa upana kwa kimo. Kwa sababu hapo pande zote ni sawa inatosha kuzidisha upande wowote mara tatu.
  • Mfano: urefu wa upande wa mchemraba ni sentimita 2 unapiga hesabu ya 23 = 2x2x2 = 8 cm3 (=sentimita mjazo).
Mchemraba ukifunguliwa

Eneo la uso[hariri | hariri chanzo]

Mchemraba huwa na pande sita sawa. Hivyo eneo la uso wake ni eneo la upande moja mara 6.

  • Mfano: Mchemraba una urefu wa sentimita mbili. Hivyo kila upande una 2x2 = 4 sm2 mara 6 = 24 sm 2.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]