Kisangani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Nembo ya Kisangani
Kiwanda cha Bralima mjini Kisangani
Mahali pa Kisangani katika JD Kongo

Kisangani ni mji mkubwa wa Kongo ya mashariki mwenye wakazi 600,000. Ni mji mkubwa wa nne wa Kongo.

Mji uko kando la mto Kongo kwenye mahali ambako mto huu mkubwa umepita maporomoko ya Bayoma na kuwa njia ya maji hadi Kinshasa.

Kisangani ilianzishwa 1883 na mpelelezi Henry Morton Stanley kama kituo cha kampuni ya mfalme Leopold II wa Ubelgiji ikaitwa baadaye Stanleyville hadi 1966. Mwanzoni utawala wa Wabelgiji ulikuwa hafifu katika mashariki ya koloni na 1888 mfanyabiashara Mswahili Tippu Tip akafanywa kuwa gavana ya mfalme Leopold II kwa sehemu za mashariki akikaa Stanleyville. Tangu 1892 Wabelgiji waliachana na Waswahili wapigana nao kivita na kuchukua utawala mkononi mwao moja kwa moja.

Kisangani iliathiriwa mara nyingi na vita hasa wakati wa uhuru wa Kongo katika miaka ya 1960 na katika vita tangu 1996 zilizosababisha anguko la dikteta Mobutu Sese Seko 1997 na kuendelea katika mapigano kati ya Rwanda, Uganda na vikundi vya Kikongo.

Hivyo hali ya uchumi ni duni ingawa mji una nafasi nzuri kijiografia.

Lugha kuu zinazojadiliwa mjini ni hasa Kilingala na Kiswahili.


Flag-map of the Democratic Republic of the Congo.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kisangani kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.