Melilla

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kisiwa cha Melilla
Ramani ya mji wa Melilla

Melilla (tamka: me-li-ya; kwa Kiarabu: مليلية, Meliliya; jina rasmi: Ciudad Autónoma de Melilla = Mji wa kujitawala wa Melilla) ni mji wa Hispania kwenye pwani ya Mediteranea unaozungukwa na eneo la Moroko upande wa bara. Umbali na Hispania bara ni takriban km 170 kuvuka bahari. Mji ulio karibu upande wa Moroko ni Nador kwenye umbali wa km 15.

Pamoja na mji wa Ceuta kisiasa ni sehemu ya Hispania na Umoja wa Ulaya, kijiografia ni sehemu ya Afrika. Moroko inadai ni sehemu ya eneo lake la kitaifa.

Watu[hariri | hariri chanzo]

Melilla ina wakazi 65,500 (mwaka 2005) katika eneo la km² 20. Zamani wakazi walio wengi walikuwa Wakatoliki wenye asili ya Hispania pamoja na Wayahudi na Waislamu Waarabu au Waberber wenye asili ya Moroko. Miaka ya nyuma idadi ya Waislamu imeongezeka ambao wengi wao wanapendelea kujiita Waberber kuliko Waarabu; Wayahudi wamepungua sana. Inasemekana ya kwamba wakazi karibu wote wanajiangalia kuwa Wahispania bila kujali kama ni Wakatoliki au Waislamu.

Uchumi unategemea uvuvi pamoja na biashara ya mpakani. Pesa rasmi ni Euro.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Historia yake ilianza zaidi ya miaka 2000 iliyopita ikaundwa kwa jina la Rusadir. Ikawa sehemu ya Dola la Roma katika jimbo la Mauretania Tingitana. Eneo lake lilipiganiwa kuanzia mwaka 429 BK kati ya wavamizi Wavandali na Bizanti.

Karibu kabla ya mwaka 700 BK Waarabu Waislamu walivamia eneo la pwani ya Moroko wakielekea Hispania. Mji ulipata jina la Meliliya ukabaki chini ya utawala wa Kiislamu hadi mwaka 1497 ulipotekwa na Wahispania.

Wahispania walifaulu kubaki na mji katika vita mbalimbali za karne zilizofuata. Mwaka 1936 vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Hispania vilianza Melilla kwa uasi wa wanajeshi dhidi ya serikali ya Jamhuri ya Hispania.

Makala hii kuhusu maeneo ya Hispania bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Melilla kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira