Sao Tome na Principe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
República Democrática de São Tomé e Príncipe
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Sao Tome na Principe
Bendera ya Sao Tome na Principe Nembo ya Sao Tome na Principe
Bendera Nembo
Wito la taifa: n/a
Wimbo wa taifa: Independência total (Uhuru Kabisa)
Lokeshen ya Sao Tome na Principe
Mji mkuu Sao Tome
0°20′ N 6°44′ E
Mji mkubwa nchini Sao Tome
Lugha rasmi Kireno
Serikali Jamhuri
Fradique de Menezes
Tomé Vera Cruz
Uhuru
 - Date
Kutoka Ureno
12 Julai 1975

currency = Dobra

Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
964 km² (ya 169)
0% (visiwa)
Idadi ya watu
 - 2005 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
169,000 (ya 173)
171/km² ()
Fedha {{{currency}}} (STD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
UTC (UTC+0)
(UTC)
Intaneti TLD .st
Kodi ya simu +239

-Sao Tome na Principe ni nchi ya visiwa katika Bahari ya Atlantiki mbele ya pwani la Afrika ya Magharibi katika Ghuba ya Guinea. Ilikuwa koloni ya Ureno hadi 1975.

Eneo lake ni hasa visiwa viwili vikubwa vya São Tomé na Príncipe pamoja na visiwa vidogo kadhaa. Sao Tome na Principe vina umbali wa 140 km kati yao vikiwa takriban 250 na 225 km kutoka pwani la Gabon. Visiwa vyote ni sehemu ya safu ya milima ya volkeni baharini. Sao Tome iko kwenye mstari wa iweta.

Jina la Sao Tome lamaanisha "Mtakatifu Thomas" kwa sababu Wareno walifika mara ya kwanza siku ya Thomas katika kalenda ya kikatoliki.

90 % za wakazi huishi kwenye kisiwa kikubwa cha Sao Tome ambacho kina urefu wa 48 km na upana wa 32 km. Hapa kuna milima ya kufikia 2.024 m juu ya UB

Kisiwa cha pili ni Principe kina urefu wa 16 km na upana wa 6 km. Mlima wake mkubwa unafikia 927 m juu ya UB.

Ramani ya Sao Tome na Pricipe

Miji[hariri | hariri chanzo]

Miji mikubwa zaidi ni (namba za 2005):

  • São Tomé: wakazi 56.1670
  • Santo Antonio: wakazi 8.239
  • Neves: wakazi 7.392
  • Santa Cruz: wakazi 6.969
  • Trindade: wakazi 6.636

Pamoja na lugha rasmi ya Kireno wakazi hutumika lugha za krioli zinazochanganya Kireno na lugha za Kibantu kama vile Saotomense (wasemaji 70.000), Principense (wasemaji 1.500) na Angolar (wasemaji 5.000).

80 % za wakazi ni Wakatoliki, takriban 10 % ni New Apostolic.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Uchumi wa visiwa ulikuwa hasa mashamba makubwa ya kakao pamoja na kahawa na mazao ya minazi.

Katika miaka ya nyuma akiba za mafuta ziligunduliwa baharini katika maeneo kati ya Sao Tome na Nigeria. Mwaka 2001 nchi zote mbili zilipatana kuendelea pamoja na utafiti wa akiba hizi. Kutokana na kazi hizi kuna matumaini ya mapato makubwa wakati ujao.

Historia[hariri | hariri chanzo]


Africa satellite plane.jpg Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Sao Tome na Principe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia