Nenda kwa yaliyomo

Togo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jamhuri ya Togo
République togolaise (Kifaransa)
Kaulimbiu: Travail, Liberté, Patrie
("Kazi, Uhuru, Taifa")
Wimbo wa taifa: Terre de nos aïeux ("Ardhi ya Mababu Zetu")
Mahali pa Togo
Mji mkuu
na mkubwa
Lomé
Lugha rasmiKifaransa
Lugha ya taifaKiewe, Kikabiye, Yoruba, Tem, Aja, Ifè, n.k.
Kabila (2023)
  • 94.4% Waafrika
  • 5.6% Wengine
Dini (2020)
 • Rais
Jean-Lucien Savi de Tové
Faure Gnassingbé
Historia
5 Julai 1884
 • Uhuru kutoka Ufaransa
27 Aprili 1960
Eneo
 • Jumlakm2 56,785 (ya 123)
 • Maji (asilimia)4.2%
Idadi ya watu
 • Kadirio la 20249,583,381
 • Msongamano125.9/km2
PLT (PPP)Kadirio la 2023
 • Jumla $25.103 bilioni
 • Kwa kila mtu $2,767
PLT (Kawaida)Kadirio la 2023
 • Jumla $9.621 bilioni (ya 157)
 • Kwa kila mtu$1,004
HDI (2022)decrease 0.547
- chini
Gini (2015)43.1
SarafuFaranga ya CFA ya Afrika Magharibi (XOF)
Majira ya saaUTC+00:00 (GMT)
Msimbo wa simu+228
Jina la kikoa.tg

Togo, rasmi Jamhuri ya Togo ni nchi katika Afrika ya Magharibi kwenye mwambao wa Ghuba ya Guinea katika bahari ya Atlantiki. Inapakana na Benin upande wa mashariki, Burkina Faso kaskazini na Ghana mashariki. Mnamo 2024 Togo ina watu takriban milioni 9.5 na kuifanya nchi ya 97 duniani kwa idadi ya watu. Mji mkuu na mkubwa zaidi ni Lome.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Togo ni nchi ndogo katika Afrika yenye km² 56,785 pekee kwa umbo la pembenne lenye urefu wa urefu wa kilometa za mraba km 550 na upana wa takriban km 130. Mwelekeo wa eneo la nchi ni kaskazini - kusini.

Humo kuna kanda zote za kijiografia za Afrika ya Magharibi kuanzia pwani yenye mchanga na misitu ya minazi kusini, vilima vya nyanda za juu katikati na savana pamoja na maeneo yabisi zaidi ya Sahel kaskazini.

Ramani ya Togo na mikoa yake.

Historia

[hariri | hariri chanzo]
Makala kuu: Historia ya Togo

Nchi hii ilianzishwa kama koloni la Togo ya Kijerumani katika pengo kati ya maeneo ya Uingereza na Ufaransa.

Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia koloni la Kijerumani liligawiwa kati ya majirani hao kama eneo lindwa chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa na baadaye ya Umoja wa Mataifa.

Mnamo Desemba 1956 wakazi wa Togo ya Kiingereza waliamua kwa kura kubaki na Ghana. Hivyo ni Togo ya Kifaransa pekee iliyopata uhuru wake mnamo Aprili 27, mwaka 1960.

Rais wa kwanza wa Togo alikuwa Sylvanus Olympio.

Nchini kuna makabila 37; kubwa zaidi ni Waewe (32%). Wazungu hawafikii 1%.

Lugha rasmi ni Kifaransa, ingawa kwa kawaida wakazi wanazungumza lugha za kikabila.

Upande wa dini, mwaka 2020 ilikadiriwa kuwa 47.8% ni Wakristo (hasa wa Kanisa Katoliki) 33% wanafuata dini asilia za Kiafrika na 18.4% ni Waislamu (hasa Wasuni).

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  • Bullock, A L C, Germany's Colonial Demands (Oxford University Press, 1939).
  • Gründer, Horst, Geschichte der deutschen Kolonien, 3. Aufl. (Paderborn, 1995).
  • Mwakikagile, Godfrey, Military Coups in West Africa Since The Sixties (Nova Science Publishers, Inc., 2001).
  • Packer, George, The Village of Waiting (Farrar, Straus and Giroux, 1988).
  • Piot, Charles, Nostalgia for the Future: West Africa After the Cold War (University of Chicago Press, 2010).
  • Schnee, Dr. Heinrich, German Colonization, Past and Future – the Truth about the German Colonies (George Allen & Unwin, 1926).
  • Sebald, Peter, Togo 1884 bis 1914. Eine Geschichte der deutschen "Musterkolonie" auf der Grundlage amtlicher Quellen (Berlin, 1987).
  • Seely, Jennifer, The Legacies of Transition Governments in Africa: The Cases of Benin and Togo (Palgrave Macmillan, 2009).
  • Zurstrassen, Bettina, "Ein Stück deutscher Erde schaffen". Koloniale Beamte in Togo 1884–1914 (Frankfurt/M., Campus, 2008) (Campus Forschung, 931).

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Serikali
Taarifa za jumla
Vyombo vya habari
Biashara
Utalii


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Togo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.