Nenda kwa yaliyomo

Sahel

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rangi ya njano inaonyesha eneo la Sahel barani Afrika.

Sahel (kutoka neno lile la Kiarabu ساحل sahil ambalo linamaanisha pwani na ni asili ya neno "Kiswahili") ni kanda nyembamba ya ardhi kavu barani Afrika kutoka Bahari ya Atlantiki hadi Bahari ya Shamu.

Ni kilometa 5,400 kwa 450-1,000 hivi kusini kwa jangwa la Sahara na kaskazini kwa eneo la misitu, ikienea kwa kiasi tofauti katika nchi zifuatazo (kutoka magharibi kwenda mashariki): Senegal, Mauritania, Mali, Burkina Faso, Aljeria, Niger, Nijeria, Chad, Sudan, Sudan Kusini, Eritrea, Kamerun, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Ethiopia.

Sahel ina tabianchi nusu-kavu ya kitropiki. Joto ni kali mwaka mzima lakini mvua chache tu (kati ya milimita 100-150 na 600 kwa mwaka) ambayo inanyesha wakati wa majira ya joto tena bila kuaminika.

Hivyo Sahel inakabili hatari kubwa ya kugeuka jangwa, pia kwa sababu wakazi wake, kwa kushindwa kulima ipasavyo, wanategemea ufugaji wa wanyama wengi mno ambao wanazidi kuharibu mazingira.

Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Sahel kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.