Jamhuri ya Afrika ya Kati
Jamhuri ya Afrika ya Kati République centrafricaine (Kifaransa) Ködörösêse tî Bêafrîka (Kisango) | |
---|---|
Kaulimbiu: "Zo Kwe Zo" (Watu wote ni watu) "Unité, Dignité, Travail" (Umoja, Heshima, Kazi) | |
Wimbo wa taifa: La Renaissance (The Renaissance) | |
Mji mkuu na mkubwa | Bangui |
Lugha rasmi | |
Kabila |
|
Dini |
|
• | Félix Moloua |
Uhuru kutoka Ufaransa | |
• Jamhuri ilianzishwa | 1 Desemba 1958 |
• Uhuru kutoka Ufaransa | 13 Agosti 1960 |
Eneo | |
• Jumla | km2 622,984 km² (ya 44) |
Idadi ya watu | |
• Kadirio la 2024 | 5,650,957 |
• Msongamano | 7.1/km2 |
PLT (PPP) | Kadirio la 2023 |
• Jumla | ▲ $5.678 bilioni |
• Kwa kila mtu | ▲ $1,109 |
PLT (Kawaida) | Kadirio la 2023 |
• Jumla | ▲ $2.760 bilioni |
• Kwa kila mtu | ▲ $539 |
HDI (2023) | ▲ 0.414 chini |
Gini (2021) | 43 |
Sarafu | Faranga ya CFA ya Afrika ya Kati (XAF) |
Majira ya saa | UTCUTC+1 (WAT) |
Msimbo wa simu | ++236 |
Jina la kikoa | .cf |
Jamhuri ya Afrika ya Kati (kwa Kisango Ködörösêse tî Bêafrîka) , ni nchi isiyo na pwani iliyoko katika katikati ya bara la Afrika. Inapakana na Chad kaskazini, Sudan na Sudan Kusini mashariki, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kusini, Jamhuri ya Kongo kusini-magharibi, na Kamerun magharibi. Ina idadi ya watu takriban milioni 5.5, ikiwa ya 117 duniani. Mji mkuu na jiji kubwa zaidi ni Bangui. Jamhuri ya Afrika ya Kati imegawanyika katika maeneo ndogo 16, pamoja na mikoa miwili maalum. Inajulikana kwa rasilimali zake asilia kama vile almasi, dhahabu, na misitu, lakini pia kwa historia ya mizozo ya kisiasa na migogoro ya silaha ambayo imeathiri maendeleo ya taifa hilo kwa muda mrefu.
Jamhuri ya Afrika ya Kati ina mchanganyiko wa makabila mengi, yakiwemo Gbaya, Banda, Mandja, Sara, na Zande, miongoni mwa mengine. Licha ya kuwa na lugha rasmi mbili—Kifaransa na Kisango—kuna zaidi ya lugha 70 zinazozungumzwa nchini humo, zikionyesha utofauti wa kitamaduni. Ukristo ndiyo dini inayotawala, ikifuatiwa na Uislamu na dini za jadi. Elimu na huduma za afya zimeathiriwa sana na mizozo ya ndani, lakini juhudi za kuimarisha huduma hizo zinaendelea kupitia usaidizi wa kimataifa.
Kwa upande wa uchumi, licha ya utajiri wa rasilimali, Jamhuri ya Afrika ya Kati ni moja ya nchi maskini zaidi duniani kwa kipato cha mtu mmoja. Shughuli kuu za kiuchumi ni kilimo, ufugaji, uchimbaji madini na misitu. Almasi ndiyo bidhaa kuu ya kuuza nje, ingawa sekta hiyo mara nyingi haijasimamiwa vizuri na imekumbwa na biashara haramu. Serikali na washirika wa kimataifa wanafanya juhudi za kuleta amani na kujenga taasisi imara za utawala ili kuwezesha maendeleo endelevu na ustawi wa kijamii.
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]
Nchi hii, hasa inashikilia mbuga ya Sudani-Guinea, lakini pia jangwa la Sahara upande wa kaskazini na msitu wa ikweta kusini.
Theluthi mbili za eneo la nchi zimetapakaa kwa mabia ya mto Ubangi unaotiririka kusini kwa Mto Kongo, na theluthi ya eneo katapakaa kwa mabia ya mto Shari, unaotiririka kusini kwa Ziwa Chadi.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Historia ya Kale
[hariri | hariri chanzo]Ukoloni wa Ufaransa
[hariri | hariri chanzo]Kwa sababu ya utapakazi wa eneo kwa mabia ya mto Ubangi na mto Shari, Wafaransa wakati wa ukoloni waliita nchi hii Ubangi-Shari (Oubangui-Chari kwa Kifaransa).
Ilipokuwa koloni la Ufaransa, Ubangi-Shari ziliwekewa mamlaka ya madaraka kama eneo la Jamii ya Wafaransa mwaka wa 1958, lakini baadaye ilipata uhuru tarehe 13 Agosti 1960.
Uhuru
[hariri | hariri chanzo]Kwa miongo mitatu kutoka uhuru, ‘Jamhuri ya Afrika ya Kati’ ilitawaliwa na serikali za mabavu zilizonyakua mamlaka bila kufuata taratibu za demokrasia.
Kwa namna ya pekee Jean-Bédel Bokassa alitawala kuanzia tarehe 31 Desemba 1965 hadi Septemba 1979, akijifanya kaisari tarehe 4 Desemba 1976.
Mwaka wa 1993, kura za kidemokrasia za kwanza zilifanywa na kumchagua Ange-Félix Patassé kuwa Rais. Lakini Rais Patassé alipinduliwa na Jenerali François Bozizé mwaka wa 2003. Baadaye huyo alishinda uchaguzi mnamo Mei 2005 na kuiongoza nchi mpaka Machi 2013 alipolazimika kukimbia.
Kati ya Novemba 2012 na tarehe 23 Julai 2014 vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipamba kwa ukatili na vinaendelea hadi mwaka 2020.
Eneo
[hariri | hariri chanzo]Jamhuri ya Afrika ya Kati imegawiwa katika maeneo 14, yanayoitwa préfectures, na pia maeneo 2 ya uchumi (préfectures economique) na mji mmoja (commune).
Maeneo hayo yamegawiwa zaidi katika wilaya 71 zinazoitwa sous-préfectures.
mikoa ni: Bamingui-Bangoran, Basse-Kotto, Haute-Kotto, Haut-Mbomou, Kémo, Lobaye, Mambéré-Kadéï, Mbomou, Nana-Mambéré, Ombella-M'Poko, Ouaka, Ouham, Ouham-Pendé, na Vakaga; maeneo ya uchumi ni Nana-Grébizi na Sangha-Mbaéré; na mji ni Bangui.
Watu
[hariri | hariri chanzo]
Nchi ina watu 4,666,368 waliogawanyika katika makabila 80, kila moja likiwa na lugha ya pekee. Ile inayowaunganisha katika mawasiliano ni Kisango, ambacho ni lugha rasmi pamoja na Kifaransa.
Kadiri ya sensa ya mwaka 2003, kati ya wakazi, 80.3% ni Wakristo (51.4% Waprotestanti na 28.9% Wakatoliki). Waislamu ni 10% na wengi wa waliobaki wanafuata dini za jadi.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Orodha ya lugha za Jamhuri ya Afrika ya Kati
- Orodha ya nchi kufuatana na wakazi
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa
- Demografia ya Afrika
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]
Habari
[hariri | hariri chanzo]- allAfrica - Jamhuri ya Afrika ya Kati kiungo cha taarifa ya habari
Uchambuzi
[hariri | hariri chanzo]- BBC News - Country Profile: Central African Republic
- CIA World Factbook - Central African Republic Ilihifadhiwa 20 Novemba 2000 kwenye Wayback Machine.
Maelekezo
[hariri | hariri chanzo]- Open Directory Project - Central African Republic Ilihifadhiwa 14 Juni 2006 kwenye Wayback Machine. directory category
- chuokikuu cha Stanford – Afrika kusini mwa sahara: Central African Republic directory category
- The Index on Africa - Jamhuri ya Afrika ya Kati Ilihifadhiwa 6 Aprili 2006 kwenye Wayback Machine. directory category
- chuo kikuu cha Pennsylvania – Masomo ya afrikar: Jamhuri ya Afrika ya Kati maelekezo
- Yahoo! - Jamhuri ya Afrika ya Kati Ilihifadhiwa 21 Aprili 2006 kwenye Wayback Machine. maelekezo
Makabila na koo
[hariri | hariri chanzo]- African Pygmies Utamaduni na muziki wa watu wa Jamhuri ya Afrika, picha na ulezaji wa ukoo.
Nchi za Afrika | ![]() |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Jamhuri ya Afrika ya Kati kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |