Cabo Verde
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Unity, Work, Progress (Umoja, Kazi, Manedeleo) | |||||
Wimbo wa taifa: Cântico da Liberdade (Wimbo wa Uhuru) | |||||
![]() | |||||
Mji mkuu | Praia | ||||
Mji mkubwa nchini | Praia | ||||
Lugha rasmi | Kireno (official) na lugha 9 za krioli | ||||
Serikali | Jamhuri Jorge Carlos Fonseca José Maria Neves | ||||
Uhuru kutoka Ureno |
imetambuliwa 5 Julai 1975 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
4,033 km² (ya 172) Kidogo sana | ||||
Idadi ya watu - Julai 2015 kadirio - 2001 sensa - Msongamano wa watu |
525,000 (ya 167) 401,343 101/km² (ya 71) | ||||
Fedha | Cape Verdean escudo (CVE )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC-1) (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .cv | ||||
Kodi ya simu | +238
- |
Cabo Verde (ing. Cape Verde) ni nchi ya visiwa katika bahari ya Atlantiki mbele ya pwani ya Afrika ya Magharibi.
Umbali wake na Senegal ni km 460.
Jiografia[hariri | hariri chanzo]
Eneo la visiwa vyake kwa jumla ni km² 4,033.
Funguvisiwa vyake ina visiwa 15 katika vikundi viwili:
- Visiwa "juu ya upepo" (Barlavento): Santo Antão, São Vicente, São Nicolau, Sal, Boa Vista na visiwa bila watu vya Santa Luzia, Branco na Razo.
- Visiwa "chini ya upepo" (Sotavento): Maio, Santiago, Fogo, Brava na visiwa bila watu vya Ilheus Secos ou do Rombo.
Miji[hariri | hariri chanzo]
Mji mkuu ni Praia katika kisiwa cha Santiago.
Miji mikubwa zaidi ni (takwimu za mwaka 2005): Praia (wakazi 113.364), Mindelo (wakazi 70.611), Santa Maria (wakazi 17.231), Pedra Badejo (wakazi 9.488) na São Filipe (wakazi 8.189).
Historia[hariri | hariri chanzo]
Hadi kufika kwa Wareno katika karne ya 15 visiwa vya Cabo Verde havikuwa na watu.
Wareno walianzisha mashamba ya miwa na kuleta watumwa kutoka bara la Afrika.
Cabo Verde ilikuwa pia kituo muhimu cha biashara ya watumwa kati ya Afrika na Amerika.
Wahamiaji kutoka Ulaya walikuwa pia Wahispania, Waitalia pamoja na Wayahudi na Waislamu waliokataliwa kukaa kwao Ureno.
Watu[hariri | hariri chanzo]
Kutokana na historia hiyo, leo idadi kubwa ya wakazi ni machotara waliozaliwa na Waafrika (waliochangia 56% ya DNA) na Wazungu (waliochangia 44%).
Lugha rasmi ni Kireno, lakini wakazi wanazungumza aina mbalimbali za Krioli iliyotokana na lugha hiyo.
Upande wa dini, walau 89.1% ya wakazi ni Wakristo, hasa wa Kanisa Katoliki (78.7%), lakini pia wa madhehebu mbalimbali ya Uprotestanti (10.4%).
Kutokana na hali ngumu ya uchumi, wananchi wanaoishi nje ya Cabo Verde ni wengi kuliko wale wanaoishi nchini. Kati ya waliohama baada ya uhuru (1975), 500,000 wanaishi Marekani na 150,000 Ureno.
Tazama pia[hariri | hariri chanzo]
- Orodha ya nchi kufuatana na wakazi
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa
- Demografia ya Afrika
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- J.Pim, C. Pierce, A.B.Watts, I. Grevemeyer, A. Krabbenhoeft (5 May 2008). "Crustal structure and origin of the Cape Verde Rise". Earth and Planetary Science Letters (Elesiever) 272: 422–428.
. http://www.earth.ox.ac.uk/~tony/watts/downloads/Pim_etal_2008.pdf.
- Carling, Jorgen (2004). "Emigration, Return and Development in Cape Verde: The Impact of Closing Borders". Population, Space and Place (John Wiley & Sons, Ltd.) 55 (10): 113–132.
. . http://www.researchgate.net/publication/227504366_Emigration_return_and_development_in_Cape_Verde_the_impact_of_closing_borders.
- Ramalho, R.; Helffrich, G.; Schmidt, D.; Vance, D. (2010). "Tracers of Uplift and Subsidence in the Cape Verde Archipelago". Journal of the Geological Society (London: Geological Society of London) 167 (3): 519–538.
. https://www.geolsoc.org.uk/en/Publications/Supplementary%20Publications/2010/~/media/Files/GSL/shared/Sup_pubs/2010/18390SupPub.ashx.
Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]
- Official website of the Government of Cape Verde
- Cabo Verde katika Open Directory Project
- Cape Verde entry at The World Factbook
- Cape Verde from State.gov
- Country Profile from BBC News
- Cape Verde entry on Encyclopædia Britannica
- Cape Verde from UCB Libraries GovPubs
- Key Development Forecasts for Cape Verde from International Futures
- Cape Verde 2012
- Amateur Radio Cabo Verde
Nchi za Afrika | ![]() |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia |
|
|
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Cabo Verde kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |