Madagaska

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
ሃግሬ ኤርትራ
Repoblikan'i Madagasikara
Republique de Madagascar
Jamhuri ya Madagaska
Flag of Madagascar Coat of Arms of Madagascar
(Kinaganaga) (Kinaganaga)
Hadabu ya Taifa: Tanindrazana, Fahafahana, Fandrosoana
(Malagasi: Nchi ya wenyeji, Rukhsa, Maendeleo) |
Location of Madagascar
Lugha za Taifa Malagasi
Kifaransa
Mji Mkuu Antananarivo
Rais
Waziri Mkuu
Hery Rajaonarimampianina
Jean Ravelonarivo
Eneo
 - Jumla
 - 0.13% Maji
Kadiriwa 45 duni
587,040 km²
Umma
 - Kadiriwa ( 58 duni )
 - Jumla (18,040,341 )
 - Umma kugawa na Eneo 31
Kadiriwa 126 duni
; (142 duni)
GDP Chumo cha uchumi
 - Jumla
 - kwa kipimo cha umma
126 kadir
$15.82 billion (223)
$900 (214)
Uhuru
 - Kadirifu
 - Barabara
Madaraka)
26 Juni 1960
Fedha Ariari
Saa za Eneo UTC +3
Wimbo wa Taifa Ry Tanindraza nay malala ô (Eh, nchi yentu asili) |
Intaneti TLD .mg
kodi za simu 261
1Lugha ya Malagasi, kulingana na katiba ndiyo lugha ya Taifa. Lugha ya Kifaransa, haijatiwa umaakini kama Lugha rasmi.
Madagaska

Jamhuri ya Madagaska inaenea katika Madagaska (pia: Bukini), kisiwa cha Bahari Hindi mashariki kwa pwani ya Afrika.

Jina[hariri | hariri chanzo]

Jina Madagaska lina maana ya "Kisiwa kikubwa" na linatokana na lugha ya wenyeji, Wamalagasi ambao waongea Kimalagasi.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Kisiwa chenyewe ni cha nne kwa ukubwa duniani.

Upekee wa kisiwa unatokana na kwamba kilimeguka kutoka India miaka milioni 88 hivi iliyopita, halafu kilibaki bila watu hadi karne ya 5 hivi BK.

Ekolojia[hariri | hariri chanzo]

Kisiwa hicho ni pia mazingira makubwa ya aina ya violezo ambayo ni asilimia 5 ya violezo vyote vya mimea na wanyama vya dunia nzima.

Asilimia 90 ya viumbe asili ni maalumu wa Madagaska, kama vile wanyama aina ya kima awali wanaoitwa lemuri, ndege ambao wasambukiza ugonjwa na mti wa mbuyu.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Bendera ya Ufalme wa Merina
Nembo ya Ufalme wa Merina

Madagaska ni kati ya maeneo ya mwisho kufikiwa na kukaliwa na binadamu.

Wa kwanza kufika walitokea visiwa vya Indonesia (kama mwaka 350-550 BK).

Baadaye tu walihamia watu kutoka bara la Afrika (mwaka 1000 hivi) na wengineo (Waarabu, Wahindi, Wazungu, Wachina n.k.).

Kuanzia mwaka 1787 hadi mwaka 1897 kisiwa kilizidi kuunganishwa kisiasa chini ya Ufalme wa Merina.

Watawala walikuwa watu kutoka familia ya Andrianampoinimerina, mwanzilishi wa taifa hilo, ambaye alikuwa ametokea katika kabila la Wamerina

Kabila hilo lilikuwa kubwa na muhimu kuliko yote 18 ya kisiwa hicho. Makazi yake yalikuwa katika uwanda wa juu wa kati lakini lilienea sehemu kubwa ya Bukini.

Wamerina walikuwa na makao makuu ya utawala wao Antananarivo; baada ya kugawiwa kwa ufalme wao mnamo 1710 kitovu cha malaka kati ya Wamerina ikahamia kwenye mlima wa Ambohimanga lakini tangu kuunganishwa kwa Wamerina mnamo 1794 mji mkuu ukulikuwa tena Atananarivo. Kutoka hapo waliweza kueneza mamlaka yao katika sehemu nyingine za kisiwa hicho.

Makabila yote ya wenyeji yalizungumza lugha moja na yalikuwa na mila na desturi zinazofanana, hivyo yaliweza kujenga umoja wa kiutamaduni uliowafanya wawe jamii moja kimsingi.

Watawala hao wa kifalme waliweza kutekeleza mambo mbalimbali kuendeleza Bukini katika vipindi vyao kabla ya kuja kwa wageni kutoka Uingereza na Ufaransa ambao kwa kiasi fulani ulidhoofisha mamlaka ya kifalme.

Kisiwa hicho hatimaye kiligeuzwa kuwa koloni la Ufaransa. Hii ni kwa kuwa, ingawa sera ya kuisasisha ya Bukini kwa namna fulani iliimarisha uwezo wa nchi hiyo wa kutetea uhuru wake, lakini kwa ujumla sera hiyo ilidhoofisha ufalme huo kwa kuongeza utegemezi wake kwa mataifa ya kigeni.

Siasa[hariri | hariri chanzo]

Miundo[hariri | hariri chanzo]

Uhusiano na nchi za kigeni[hariri | hariri chanzo]

Watu[hariri | hariri chanzo]

Mtoto wa Kimalagasi anayeonyesha kuwa na mchanganyiko wa damu.

Mwaka 2012 idadi ya wakazi ilikadiriwa kuwa milioni 22. Wenyeji wengi wana mchanganyiko wa damu: DNA inaonyesha kuwa wakazi wa kwanza kutoka Indonesia wameichangia asilimia 50 hivi na Waafrika vilevile. Wanaoishi sehemu za ndani ni wa Kiindonesia zaidi, wakati wale wa pwani ni wa Kiafrika zaidi.

Lugha[hariri | hariri chanzo]

Lugha rasmi za Madagaska ni Kimalagasi na Kifaransa (angalia pia orodha ya lugha za Madagaska).

Dini[hariri | hariri chanzo]

Nchini Madagaska kuna dini za jadi (52% hivi), Ukristo (41%, Waprotestanti wakiwazidi kidogo Wakatoliki), Uislamu (7% hivi) n.k.

Utamaduni[hariri | hariri chanzo]

Pamoja na kutokea mazingira tofauti sana, Wamalagasi wamechanganyikana sana na kuwa na utamaduni na lugha aina moja, ya Kiindonesia zaidi.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

      . http://books.google.com/books?id=Szvr5hUtD5kC&printsec=frontcover.
      .
      . http://books.google.com/books?id=3mE04D9PMpAC&printsec=frontcover.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Majiranukta kwenye ramani: 20°S 47°E / 20°S 47°E / -20; 47


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia
Africa satellite plane.jpg Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Madagaska kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.