Nenda kwa yaliyomo

Antananarivo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Antananarivo kati, pia ziwa anosy


Jiji la Antananarivo
Nchi Madagaska
Mkoa Analamanga
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 1 403 449
Tovuti:  www.antananarivo.mg
Mahali Antananarivo iko Madagaska
Antananarivo, Madagaska

Antanànarìvo (matamushi [An/ta/na/ri/vo], Umma 1,403,449 (2001 sensa), ni Mji Mkuu wa Madagaska, kwa Mkoa wa Antananarivo.

Pia mji huu wajulikana kwa jina la Kifaransa kama Tananarive ama kwa kifupi ni Tana. Antanànarivo iko kati ya kisiwa kulingana na usabaa wa kisiwa, lakini ni maili 90 kutoka pwani ya magharibi. Mji mwenyewe una kituo cha amri, kinachojengwa juu ya milima na mabonde marefu yenye miamba na nyembamba. Hii milima na mabonde imesambaa kusini na kaskazini kama 2-½ maili, ikigawa kaskazini kwa njiapanda, na kukwea mahali juu zaidi pakiwa 690 ft. juu ya viwanja dhihirifu za mchele upande wa magharibi, ambazo zenyewe zimo 4060 ft. juu ya usawa wa bahari. Mji huu ni mji mkubwa nchini Madagaska na ni kituo cha amri ya serikali, mawasiliano, na kituo cha uchumi. Mahali Mji huu uko ni 18°55' Kusini, 47°31' Magharibi (-18.916667, 47.516667) [1] Archived 25 Machi 2011 at the Wayback Machine., Maili 135 Magharibi-kusini magharibi ya Tamatave, ni bandari ya kisiwa hiki, ambayo imeungwa kwa reli, na kwa maili 60 kwa pwani kuna jahazi za kusafirisha. Viwanda vyahusu utolezi wa kuunda sigara, na nguo.

Antananarivo ilianza pengine mwaka wa 1625. Kwa muda mrefu machifu wa kijiji cha Hova pekee, waliweza kujipa Uhuru kutoka sehemu nyingine za Madagaska, na kwa hivyo Antananarivo kuwa mji wa maana, na baadaye kuwa mji asili kwa kuongezeka wa wakazi 80,000. Mwaka wa 1793 mji huu ulifanywa uwe mji mkuu wa Wafalme wa Merina. Kushindwa kwa Mfalme Radama (wa kwanza) iliifanya Antananarivo iwe mji mkuu wa Madagaska yote. Mwaka wa 1869 majengo yote kwa mji asili, yalikuwa ya mbao ama nyazi, na hata hivyo mji wenyewe ulikuwa na Jumba za kifalme kubwa, kubwa zaidi ikiwa 120 ft. kwenda juu. Hili jumba lilataji sehemu ya bonde la kati; na jumba hili kubwa zaidi, dari na minara yake imepaa juu, na kwahivyo kuonekana kutoka sehemu zote.

Kutoka uwanzo wa mawe na tofali, mji wote umejengwa na sasa kuna majengo ya aina nyingi na ya kuhifadhi, Jumba la Kifalme, Nyumba ambazo zilikuwa za Waziri mkuu na masharifu, makazi ya kifaransa, Kathidro ya Aglikan na Katoliki wa Kiromathe, Kanisa kadhaa za mawe na nyingine za matofali, Chuo, Shule, hospitali, Mahakama ya Sheria na Majengo ya Serikali, na nyumba nyingine za kuishi.

Mji huu ulitekwa na Wafaransa mwaka wa 1895 na kuwekwa kwa koloni ya eneo ya Madagaska. Kutoka ukoloni wa ufaransa barabara njema zilitengenezwa kwa mji, ngazi pana za kupaa kwa eneo ya mabonde zimeunganisha sehemu zile ziko kwa ukwea zaidi na ziwezi kuundwa barabara za kawaida, na sehemu ya kati inayoitwa Andohalo, ni sehemu nzuri sana, ambayo inajia za kutembea na daraja za ukwea ambazo ni shamba za maua na miti. Hifadhi zimewekwa karibu na makazi ya watu, na upandaji wa miti na mashamba ya uhifadhi eneo nyingi za mji zaipatia mji urembo na utulifu. Maji ya patikana kwa chemchem chini ya milima lakini maji mengi yatoka kwa mto Ikopa, ambao mto huo wapitia kando ya Mji kusini na magharibi. Mji wenyewe umelindwa na Vigome viwili ambazo zilijengwa kwa mlima mashariki na kusini-magharibi. Pia kathidro ya Anglikani na katoliki ya kiroma, kuna Kanisa zaidi ya hamsini mjini na eneo za mji, na hata Miskiti za kiislamu. Antananarivo ni nyumbani kwa Chuo Kikuu cha Madagascar na Chuo cha Ambatobe (Collège Rural d'Ambatobe).

Antanànarìvo ya maanisha "Mji wa Maelfu" (arivo=Elfu). Miaka ya ukoloni na hata miaka iliyofuatia Uhuru wa Madagaska, Antananarivo iliitwa 'Tananarive.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Antananarivo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: