Nenda kwa yaliyomo

Historia ya Madagaska

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Historia ya Madagaska inahusu Kisiwa kikubwa cha Bahari ya Hindi mkabala wa Afrika Mashariki ambalo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Madagaska.

Mfalme Andrianampoinimerina (1787-1810)
Bendera ya Ufalme wa Merina
Nembo ya Ufalme wa Merina

Madagaska ni kati ya maeneo ya mwisho kufikiwa na kukaliwa na binadamu duniani.

Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa watu walitokea visiwa vya Indonesia (kama mwaka 350-550 BK).

Katika karne zilizofuata walifika wahamiaji Wabantu kutoka bara la Afrika (mwaka 1000 hivi) na wengineo (Waarabu, Wahindi, Wazungu, Wachina n.k.).

Kuanzia mwaka 1787 hadi mwaka 1897 kisiwa kilizidi kuunganishwa kisiasa chini ya Ufalme wa Merina.

Watawala walikuwa watu kutoka familia ya Andrianampoinimerina, mwanzilishi wa taifa hilo, ambaye alikuwa ametokea katika kabila la Wamerina

Kabila hilo lilikuwa kubwa na muhimu kuliko yote 18 ya kisiwa hicho. Makazi yake yalikuwa katika uwanda wa juu wa kati lakini lilienea sehemu kubwa ya Bukini.

Wamerina waliweka makao makuu ya utawala wao mjini Antananarivo; kutoka hapo waliweza kueneza mamlaka yao katika sehemu nyingine za kisiwa hicho.

Makabila yote ya wenyeji yalizungumza lugha moja na yalikuwa na mila na desturi zinazofanana, hivyo yaliweza kujenga umoja wa kiutamaduni uliowafanya wawe jamii moja kimsingi.

Watawala hao wa kifalme waliweza kutekeleza mambo mbalimbali kuendeleza Bukini katika vipindi vyao kabla ya kuja kwa wageni kutoka Uingereza na Ufaransa ambao kwa kiasi fulani ulidhoofisha mamlaka ya kifalme.

Kisiwa hicho hatimaye kiligeuzwa kuwa koloni la Ufaransa. Hii ni kwa kuwa, ingawa sera ya kuisasisha ya Bukini kwa namna fulani iliimarisha uwezo wa nchi hiyo wa kutetea uhuru wake, lakini kwa ujumla sera hiyo ilidhoofisha ufalme huo kwa kuongeza utegemezi wake kwa mataifa ya kigeni.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Madagaska kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.