Historia ya Liberia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Historia ya Liberia inahusu eneo la Afrika Magharibi ambalo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Liberia.

Liberia ni nchi iliyoundwa na makabila 16 ya asili nchini humo na wahamiaji Weusi toka Marekani na Karibi (5%), mbali na machotara wa aina mbalimbali.

Wamarekani Weusi hao walikuwa watumwa waliopata uhuru ambao kwa kushirikiana na chama cha American Colonization Society waliunda taifa hili na kutangaza uhuru wa nchi hiyo tarehe 26 Julai 1847.

Wamarekani Weusi hao waliichukulia nchi hiyo kama nchi ya ahadi kutokana na asili yao kuwa Afrika, ambako ndiko mababu zao walikotokea kabla ya kupelekwa utumwani Marekani.

Hata hivyo, wahamiaji hao waliendelea kujitambulisha kama Wamarekani na hawakujenga mahusiano ya karibu na wenyeji.

Alama za taifa hili (bendera, kauli mbiu, na nembo) na hata muundo wa serikali vilikuwa vikionyesha mahusiano ya karibu kati ya nchi hizo mbili.

Liberia ilikuwa katika vita ya wenyewe kwa wenyewe kati ya miaka 1989-1996 na 1999-2003.

Hivi karibuni umefanywa kwa mara ya pili uchaguzi kwa amani na kuweza kumchagua George Weah kushika (2018) nafasi ya Ellen Johnson-Sirleaf, mwanamke wa kwanza kuwa Rais barani Afrika.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Liberia kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.