Historia ya Togo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Historia ya Togo inahusu eneo la Afrika Magharibi ambalo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Togo.

Nchi ilianzishwa kama koloni la Togo ya Kijerumani katika pengo kati ya maeneo ya Uingereza na Ufaransa.

Baada ya Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia koloni la Ujerumani liligawiwa kati ya majirani hao kama eneo lindwa chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa na baadaye ya Umoja wa Mataifa.

Mnamo Desemba 1956 wakazi wa Togo ya Kiingereza waliamua kwa kura kubaki na Ghana. Hivyo ni Togo ya Kifaransa pekee iliyopata uhuru mwaka 1960.

Rais wa kwanza alikuwa Sylvanus Olympio.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Togo kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.