Ellen Johnson-Sirleaf

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ellen Johnson-Sirleaf

Ellen Johnson-Sirleaf (alizaliwa 29 Oktoba 1938 nchini Liberia) amekuwa rais wa kwanza mwanamke barani Afrika baada ya kushinda katika uchaguzi wa mwaka 2005. Johnson-Sirleaf ameshika nyadhifa mbalimbali serikalini na katika mashirika ya kimataifa. Baada ya kumaliza masomo katika chuo kikuu cha Harvard, alifanya kazi katika serikali ya Rais William Tolbert mwaka wa 1970 akiwa ni Waziri wa Fedha.

Johnson amekuwa Rais wa kwanza mwanamke barani Afrika. Hata hivyo yeye sio mwanamke wa kwanza kuongoza nchi barani Afrika. Malikia Zauditu wa Ethiopia aliongoza nchi yake kwa miaka 13 toka mwaka 1917 hadi 1930. Ruth Perry ni mwanamke wa kwanza Afrika kuwa mkuu wa nchi pale alipokuwa mwenyekiti wa urais wa pamoja wa jamhuri ya Liberia toka mwaka 1996 hadi 1997.

Johnson-Sirleaf alihukumiwa kifungo cha miaka kumi jela mwaka 1985 baada ya kushutumu utawala wa kijeshi nchini humo katika kampeni zake za kugombea ubunge. Alitumia kifungo hicho kwa muda mfupi kabla ya kuachiliwa na baadaye kukimbilia uhamishoni hadi aliporudi mwaka 1997 akiwa anafanyia kazi Benki ya Dunia na Citibank.

Johnson-Sirleaf alimuunga mkono Charles Taylor wakati wa mapinduzi yake dhidi ya Jenerali Samuel Doe lakini baadaye alikuja kuwa mpinzani wake mkubwa na hata kugombea urais dhidi yake mwaka 1997. Taylor alimwandana na hata kumpeleka mahakamani kwa madai ya kuhusika na hujuma za kihaini.

Uchaguzi wa urais mwaka 2005 ulirudiwa baada wagombea urais kutopata kura za kutosha. Katika raundi ya kwanza Johnson-Sirleaf alikuwa wa pili, wa kwanza alikuwa ni mpinzani wake mkubwa George Weah. Katika raundi ya pili ya uchaguzi, Johnson-Sirleaf alitangazwa kuwa mshindi. Hata hivyo, George Weah amepeleka mashtaka mahakama kuu akidai kuwa uchaguzi haukuwa wa haki.

Mnamo Desemba 2021, James Sirleaf mmoja wa wana wa Ellen Sirleaf alikufa katika makazi yake huko Liberia chini ya hali isiyojulikana.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Ellen Johnson Sirleaf alizaliwa mjini Monrovia, mji mkuu wa Liberia, na elimu ya wazazi. Kabila lake ni nusu Gola kutoka upande wa baba yake, na robo Kru na robo Kijerumani kutoka upande wa mama yake. Babake Sirleaf Jahmale Carney Johnson, alikuwa mzaliwa wa Liberia wa kwanza kuweza kukaa katika mbunge la taifa. Sirleaf alisoma maswala ya uchumi na akaunti katika Chuo Afrika Magharibi mjini Monrovia. Aliolewa na James Sirleaf akiwa na miaka 17 tu na kuhamia Marekani katika mwaka wa 1961 ambapo aliendelea na masomo yake katika chuo kikuu cha Colorado na kuhitimu na shahada ya digri. Alisomea maswala ya uchumi na sera za umma katika chuo Chuo Cha Maswala Ya Serikali ya John F. Kennedy, mjini Harvard katika miaka ya 1969 na 1971 na kupata shahada ya maswala ya serikali. Kisha alirudi Liberia na kufanya kazi chini ya rais William Tolbert. Alikuwa naibu waziri wa fedha kati ya mwaka wa 1972 na 1973. Alikuwa waziri wa fedha toka mwaka wa 1979 hadi Aprili 1980. Aliweza kuwa naibu mwenyekiti wa benki ya CitiBank mjini Nairobi, Kenya kutoka mwaka wa 1983-1985. Aliwahi kufungwa mafungo ya nyumbani na Samule Doe aliyepindua serikali kwa kutangaza nia ya kugombea urais. Baadaye alienda uhamishoni. Kati ya miaka ya 1986-1992 alikuwa makamu wa rais na mwanachama wa bodi ya benki ya Equator, Washington, DC. Kati ya miaka ya 1988-1999 alikuwa mbunge wa bodi ya wakurugenzi wa Taasisi ya Synergos. ALigombea urais kwa tiketi ya chama ya maungano(Unity Party) katika mwaka wa 1997 na kuwa

Urais[hariri | hariri chanzo]

Ndiye rais wa sasa wa Liberia. Alimshinda alikuwa mwanasoka mashuhuri George Weah na zaidi ya asilimia ishirini katika uchaguzi wa mwaka wa 2005. Uzinduzi ulifanyika tarehe 16 Januari 2006 na ulihudhuriwa na wageni mashuhuri wakiwemo aliyekuwa waziri ya maswala ya kigeni wa Marekani, Condeleeza Rice, Laura Bush na Mitchelle Jean. Katika mwaka wa 2005 alianzisha tume ya ukweli na maridhiano ambayo ilitoa ripoti yake katika mwaka wa 2009.

Hatamu za Uongozi[hariri | hariri chanzo]

 • 1972–1973:: Naibu Waziri wa Fedha wa Liberia
 • 1979–1980: Waziri wa Fedha wa Liberia
 • 1982-1985: Makamu wa Rais wa Kanda ya Afrika Ofisi ya Citibank, Nairobi
 • 1986-1992: Makamu wa Rais na mwanachama wa bodi ya beni ya Ikweta, Washington, DC
 • 1988-1999: Mbunge wa bodi ya wakurugenzi wa Taasisi ya Synergos
 • 1992-1997: Mkurugenzi wa Mpango wa Maendeleo ya Umoja wa mataifa Ofisi za bara Afrika
 • 1997: Rais mgombea wa chama cha Umoja(Unity Party)
 • 2004-2005: Mwenyekiti wa Tume ya Mageuzi ya Utawala Bora
 • 2005:Mgombea urais kwa tikiti ya chama ya umoja
 • 2006 hadi leo: Rais wa Liberia

Nyadhifa nyingine zilizotangulia[hariri | hariri chanzo]

 • Mwanachama mwanzilishi wa Taasisi ya Kimataifa kwa Wanawake katika uongozi wa kisiasa
 • Mwanachama wa bodi ya ushauri wa kisasa wa Kukuza Uchumi na Uwekezaji Afrika Kampuni
 • Afisa mwandamizi wa mkopo wa Benki ya Dunia
Wikimedia Commons ina media kuhusu: