Ruth Perry

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Ruth Fahnbulleh Perry alikuwa ni kiongozi wa Liberia toka 3 Septemba 1996 hadi 2 Agosti 1997. Aliongoza nchi hiyo kama mwenyekiti wa Baraza la Taifa ambalo liliongoza nchi hiyo kufuatia kuangushwa kwa Sajenti Samuel Doe na mwisho wa urais wa Amos Sawyer. Perry alikuwa ni mwanachama wa chama cha National Democratic Party cha Liberia.

Baada ya uchaguzi wa Urais hapo Julai 1997, Perry alimwachia madaraka Charles Taylor.