Historia ya Kamerun

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Historia ya Kamerun inahusu eneo la Afrika ya Kati ambalo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Kamerun.

Historia ya awali[hariri | hariri chanzo]

Katika karne za BK Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi walianza uenezi wao kutoka huko kwenda kutawala maeneo mengi ya Afrika ya Kati, Kusini mwa Afrika na Afrika Mashariki.

Wakati wa ukoloni[hariri | hariri chanzo]

Kamerun ilikuwa koloni la Ujerumani hadi Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Baada ya Ujerumani kushindwa vita, nchi ikagawiwa kati ya Uingereza na Ufaransa chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa kama eneo la kukabidhiwa.

Tangu uhuru hadi leo[hariri | hariri chanzo]

Mwaka wa 1960, Wafaransa waliacha Kamerun ikawa nchi huru, na kuungana na sehemu ya kusini ya Kamerun ya Kiingereza mwaka 1961 kuunda Shirikisho la Jamhuri ya Kamerun.

Baadaye jina likabadilishwa kuwa Jamhuri ya Muungano ya Kamerun mwaka wa 1972, halafu tena Jamhuri ya Kamerun (kwa Kifaransa République du Cameroun) mwaka wa 1984.

Badiliko hilo la muundo wa nchi kuacha mfumo wa shirikisho na kuwa jamhuri ya muungano inakazia zaidi matumizi ya lugha ya Kifaransa ingawa Kiingereza bado ni moja ya lugha rasmi. Hapo sehemu ya Wakamerun wanaotumia lugha ya Kiingereza walijisikia kuwa wananyimwa haki zao.

Tangu mwaka 2016 upinzani wa watu wa magharibi ulijibiwa kwa ukali zaidi na hii imeleta upinzani wa wanamgambo wenye silaha wanaoshambulia polisi na jeshi la serikali kuu. Tangu mwaka 2017 wapinzani wamedai uhuru wa sehemu yenye lugha ya Kiingereza wakidai kuundwa kwa nchi ya Ambazonia.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Hourglass.svg Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Kamerun kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.