Historia ya Eritrea

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Historia ya Eritrea kama eneo la pekee jinsi ilivyopata uhuru mwisho wa karne ya 2o ilianza na ukoloni wa Italia. Hadi karne ya 19 maeneo ya Eritrea yalikuwa sehemu ya Ethiopia. Pwani lilikaa karne nyingi chini ya utawala wa Uturuki au baadaye Misri kama nchi zenye nguvu kwenye Bahari ya Shamu.

Mwanzo wa ukoloni wa Italia[hariri | hariri chanzo]

Katika Novemba 1869 kampuni ya biashara ya Kiitalia ya Rubattino ilinunua bandari ya Assab kutoka usultani wa Afar. Ilitafuta kituo kwa meli zake zilizoanza kupita katika bahari ya Shamu baada ya kufunguliwa kwa Mfereji wa Suez mwaka uleule.

Serikali ya Misri ilipinga mapatano haya kwa sababu ilidai eneo lilikuwa chini ya amri yake. Makubaliano hayakufikiwa hadi 1882 serikali ya Italia ilipochukua mali ya kampuni moja kwa moja kama koloni yake ya kwanza katika Afrika.

Tangu kuporomoka kwa uatawala wa Misri nchini Sudan baada ya vita ya Al-Mahdi Misri ilijiondoa pia katika pwani la kusini ya bahari ya Shamu. Italia ilitumia nafasi hii na 5 Februari 1885 ilipeleka wanajeshi mjini Massawa na kuitangaza kuwa koloni yake. Waitalia waliendelea kuunganisha maeneo yao ya Assab na Massawa. Baadaye walijaribu kupanusha utawala wao kutoka tambarare za pwani hadi nyanda za juu zilizokuwa chini ya Dola la Ethiopia.

Negus Yohanne IV hakufurahia kufika kwa Italia kwa sababu aliamini ya kwamba Massawa iliahidiwa kwake baada ya kuwasaidia Wamisri kujiokoa mbele ya jeshi la Al-Mahdi. Hivyo upanuzi wa Italia katika nyanda za juu ulikutana na upinzani. Tarehe 26 Januari 1887 jeshi la Waitalia 587 walioelekea kaskazini lilishambuliwa karibu na Massawa kwenye kijiji cha Dogali na kushindwa na Ras Alula aliyekuwa mtemi chini ya Negus ya Ethiopia. Waitalia walipaswa kuongeza wanajeshi 13,000 ili kuhakikisha utawala wao.

Mkataba wa Wuchale na mapigano ya Adowa[hariri | hariri chanzo]

Baada ya Yohann IV kufariki katika mapigano na jeshi la Al-Mahdi, Waitalia walichukua nafasi hii ya kuiingia nyanda za juu za Tigray na kujenga vituo vyao huko. Mfalme mpya Menelik II tarehe 2 Mei 1889 alitia sahihi kwenye mkataba wa Wuchale iliyokubali utawala wa Italia juu ya kanza ya pwani pamoja na maeneo kadhaa ya nyanda za juu za Tigray.

Waitalia walijaribu kumdanganya Negus katika mkataba huu kwa kuingiza maneno katika nakala ya Kiitalia ya mkataba huu yaliyosema "Ethiopia itakuwa chini ya ulinzi wa Italia". Menelik baada ya kuelewa haya alikana mkataba. Italia ilijibu kwa kuvamia Ethiopia kwa jeshi kubwa. Jeshi hili lilishindwa na Waethiopia katika mapigano ya Adowa tar. 1 Machi 1896. Italia ilipaswa kukubali uhuru wa Ethiopia katika mkataba wa amani 26 Oktoba 1896. Ethiopia ilikubali mamlaka ya Italia juu ya koloni yake katika kaskazini.

Koloni ya Eritrea[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kumaliza mashindano na Ethiopia Italia tarehe 1. Januari 1890 iliunganisha maeneo yake yote katika koloni iliyoitwa Eritrea kufuatana na jina la kale "Bahari ya Eritrea".

Katika kipindi hiki cha utawala wa kikoloni Eritrea ilitokea kama jamii na eneo la pekee. Koloni ya Eritrea iliunganisha maeneo matatu yenye tabia za pekee:

  • kanda la pwani lililokuwa na historia ndefu ya biashara na mawasiliano na Uarabuni ng'ambo ya Bahari ya Shamu
  • kanda la sahel katika kaskazini-magharibi lililowahi kuwa sehemu ya Sudan
  • kanda ya nyanda za juu liliwahi kuwa sehemu ya utamaduni wa Watigray Wakristo

Italia ilianzisha miradi ya kufanya Eritrea chanzo cha malighafi kwa ajili ya uchumi wa Italia. Kijiji cha Asmara katika nyanda za juu kilikuwa mji mkuu wa koloni na kupanushwa kuwa mji kwa ajili ya walowezi Waitalia. Asmara ilipambwa na majengo mazuri ya kisasa. Katika miaka ya 1930 idadi ya motokaa zilizoendeshwa Asmara ilishinda idadi ya magari ya binafsi mjini Roma. Urithi huu wa majengo umekuwa sababu ya kuingiza Asmara katika orodha ya Urithi wa dunia ya UNESCO.

Waitalia walipanga na kujenga miji mingine kama vitovu vya biashara, mabandari, vituo vya kijeshi au vya kiuchumi.

Idadi ya wakazi wote ilikadiriwa kuwa takriban 200,000 mwaka 1890. Idadi hii iliongezeka haraka kufikia zaidi ya 600,000 mnamo 1939. Mabadiliko makubwa yalitokea hasa katika nyanda za juu ambako walowezi Waitalia walianzisha mashamba yao na miji mikubwa zaidi ilijengwa.

Idadi ya wasemaji wa Kitigrinya iliongezeka kutoka asilimia 35 mwaka 1905 kuwa asilimia 54 mwaka 1939.

Mwisho wa vita kati ya vikundi mbalimbali na kupatikana kwa huduma za kiafya pamoja na kuongezeka kwa upatikanaji wa chakula vyote vilichangia katika kuonegezeka kwa idadi ya watu.

Kati ya mabadiliko makubwa ulikuwa ujenzi wa barabara na reli kati ya Massawa, Asmara, Keren na Agordat. Viwanda kadhaa vilianzishwa pia migodi ya kuchimba mawe au madini. Sehemu za Waeritrea waliingia katika maisha ya ajira ya kibepari. Hivyo maarifa ya wakazi wa Eritrea hasa katika nyanda za juu ilikuwa tofauti na wenzao katika Ethiopia penyewe walioendelea kuishi chini ya utaratibu wa kimakabaila. Waeritrea walisukumwa katika maisha ya kisasa na uchumi wa fedha. Hadi 1940 Eritrea ilikuwa tayari na tabaka ya wafanyakazi wa viwandani na katika miji pia tabaka ya wasomi wenye elimu ya kisasa.

Baada ya Mussolini kushika serikali siasa ya Kiitalia ilibadilika. Wafashisti walidharau Waafrika na kuanzisha siasa ya ubaguzi wa rangi. Wenyeji walipewa tu shughuli za duni kabisa katika utumishi wa serikali.

Itali ya kifashisti ilifanya mipango ya kulipizia kisasi mapigano ya Adowa ikiandaa vita dhidi ya Ethiopia. Vita ilianza 1935 kutoka ardhi ya Eritrea. Silaha mpya za Italia zilishinda jeshi la Negus Ethiopia yote ikawa koloni ya Italia.

Kipindi cha Kiingereza[hariri | hariri chanzo]

Waitalia walishindwa katika Vita Kuu ya pili ya Dunia mwaka 1941. Waingereza waliteka Ethiopia pamoja na Eritrea. Waingereza walitawala Eritrea hadi 1952. Mwaka huu Umoja wa Mataifa ulikabidhi Eritrea kwa Ethiopia kama eneo la pekee lenye serikali na bunge lake.

Mfalme wa Ethiopia, Mfalme Haile Selassie hakupendezwa na utaratibu huu alilenga kuunganisha Eritrea tena na Ethiopia na kwa mbinu mbalimabli alipata kura ya bunge la Eritrea ya kujivunja na kuwa jimbo la Ethiopia.

Vita ya kupigania uhuru[hariri | hariri chanzo]

Baada ya tukio hili vikundi vya wanamigambo walienda porini kupigania kwa silaha uhuru ya Eritrea.

Vita ya Uhuru wa Eritrea ilitambakaa mwaka 1974 baada ya Ufalme Kupenduliwa na Makisti kuingia na rundo ya Jeshi iliyoitwa Derg kuchukuwa mamlaka, na badaye kuvamiya Eritrea. Ukorofi wa serikali ya Mengistu Haile Mariam ilifanya mengi kuongeza watumaini wa Uhuru wa Eritrea kati ya karne 1980.

Ukombozi wa Eritrea ulitegemea rundo ya Eritrean Liberation Front (ELF), ambayo piya inaitwa "Jebha", na Eritrean People's Liberation Front (EPLF), ambaye piya inaitwa "Shaabia". ELF ilikuwa na Waislamu wengi wa pwani na waifadhi wa tedo za wananchi,na EPLF wengi wakristo kutoka nyanda za juu, milimani za Tigrayi waamini Makisti-ULenin. ELF ilisaidiwa na wafadhili wa Arabu, na EPLF kutoka nchi za kikomunisti zilizokuwa upande wa Urusi, lakini badaye nchi hizo zikapenduka EPLF na kusaidia Derg ya Mengistu Hail Mariam. ELF na EPLF hazikuweza kufanya kazi pamoja na kwa hivyo EPLF ikaimaliza ELF na kuendelea kutafuta Uhuru.

Vita ya Uhuru iliisha mwaka 1991, Eritrean na waasi Waethiopia kutoka Tigray walishinda jeshi ya Ethiopian, na serikali ya Derg ikaanguka. miaka miwili baadaye.

Eritrea huru[hariri | hariri chanzo]

Baada kura ya wakazi wa Eritrea uhuru wa nchi ilitangazwa tarehe 24 Mei 1993. Awali uhusiano na serikali mpya ya Ethiopia ulikuwa mzuri lakini baada ya miaka ya kwanza ulianza kuzorota. 1998 kulitokea vita kati ya Eritrea na Ethiopia uliokwisha na ushindi wa Ethiopia. Wanajeshi la kulinda amani ya UM wanajaribu kutunza hali ya kutopigana.

Kiongozi wa EPLF, Isaias Afewerki, akawa Rais. Eritrea (EPLF or Shaebia), ikawa chapa pekee kinachotawala eritrea kwa sheria na kupendua jina People's Front for Democracy and Justice (PFDJ).

Mwaka 1998, vita ya mpaka na Ethiopia ilileta kifo kwa wanajeshi wengi kwa nchi zote mbili, na Eritrea Uchumi wake ukafifia na wananchi waka hangaika sana. Umma wa nchi ukanza uhamaji na uchummi kukosa maendeleo. Eritrea ni nchi moja yazo Afrika ambapo kuna shida ya mobomu ya arthi. Serikali ya Ethiopia, iliwafukuza wa Eritrea ambao waiishi Ethiopia ama watu waliokuwa na utamaduni wa Eritrea baada ya vita na Eritrea. Hii iliwaletea Eritrea shida na wahamaji.

Hata baada ya Kuonyesha maendeleo kidogo kwa uchumi na siasa serikali ya Eritrea inanyanyasa magazeti na waandishi na piya kunyanyasa watu kwa siasa. Serikali yenyewe hata haijaweza kuweka Katiba mpya na Kuleta Kura ya kidemocrasia. Baadaye, serikali ya Eritrea imeweza kusisitiza desturi ya ukoloni wa Waitaliano ambayo inaitaji kanisa na Dini kujiandikisha kwa serikali na kupewa ruhusa wa kuhubiri Dini. Dini zilizopewa ruhusa na serikali ni Eritrean Orthodox Church, Roman Catholic Church, na Kanisa la Mekane Yesus (Waluteri), na Uislamu. Hizo kanisa zingine zote hasa, wafundamentalisti, Wainjili Protestanti wakristo, hasa wamefinyiliwa kote nchini.

Vita vya Eritrea na Ethiopia ziliisha mwaka wa 2000 na mwagano wa kushauriana unao julikana kama Mwagano wa Algiers. Moja wapo ya makubaliano ilikuwa kuanzisha endesho la Muungano wa kimataifa la kuweka amani, abayo inajulikana kama, Muungano wa Kimataifa wamisheni ya Eritrea na Ethiopia (UNMEE); Waweka amani 4,000 wa UM wa mebaki kutoka mwezi Agosti 2004.

Makubaliano mengine ya Algiers ilikuwa kuanzisha usawanisho wa mwisho wa mpaka uliyo bishaniwa kati ya Eritrea na Ethiopia. Komisheni iliyo kuwa madaraka, iliyo itwa washiriki wa Muungano wa Kimataifa wa komisheni ya mpaka wa Ethiopia na Eritrea(EEBC), baada ya somo ndefu, walikata maamuzi ya mwisho Aprili 2002, lakini maamuzi yao ikakataliwa na Ethiopia. Kutoka Oktoba 2005 bishano la mpaka bado limebaki kwa swali, hata kama umaakini na mkomo wa vita unaangaliwa kwa kazo.