Nenda kwa yaliyomo

Derg

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Derg ni neno la Kiethiopia kwa ajili ya "kamati" au "halmashauri". Inamaanisha hasa kikundi cha wanajeshi waliompindua Kaisari Haile Selassie mwaka 1974 na kushika mamlaka ya serikali nchini Ethiopia.

Derg ilikuwa kamati ya wawakilishi kutoka sehemu mbalimbali za jeshi kama jeshi la nchi kavu, wanamaji, wanaanga na polisi. Derg ilitawala hadi 1987.

Kati ya 1975 na 1977 watu makumi elfu waliuawa hovyo kwa amri za Derg.

Mwenyekiti na kiongozi mkuu wa Derg alikuwa Mengistu Haile Mariam.

1987 Derg ilikabidhi madaraka kufuatana na katiba mpya na Ethiopia kutangazwa kuwa jamhuri ya kisoshalisti na Mengistu rais wake.