Ubaguzi wa rangi

Ubaguzi wa rangi ni kitendo cha kuthamini au kutenga binadamu kwa misingi ya rangi za ngozi. Ubaguzi wa rangi ulikuwa maarufu sana katika nchi kama Afrika Kusini kwa jina la "apartheid" na Marekani kwa jina la "segregation" ambapo huko Waafrika walikandamizwa kutokana na rangi yao katika kupata huduma mbalimbali za kijamii na kimaendeleo.
Wakati wa ukoloni, rangi ilitumika kama msingi wa utoaji huduma muhimu mfano: shule, matibabu na haki nyingine za kibinadamu. Rangi nyeusi ilipewa hadhi ya chini zaidi.
Siku hizi katika karibu nchi zote, sheria zinapinga ubaguzi wa rangi. Lakini katika nchi nyingi bado kuna wabaguzi wachache ambao wanavunja sheria kwa kuendelea kubagua. Kwa mfano, kuna wabaguzi wanaobagua Watu weusi nchini Marekani, nchini China, nchini India na katika nchi za Ulaya.
Ubaguzi dhidi ya Waafrika, haswa wale wenye asili ya Kiafrika wanaoishi nje ya bara, unashutumiwa mara kwa mara lakini haujakoma.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Mkutano wa Kimataifa Dhidi ya Ubaguzi (Kiingereza)
| Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ubaguzi wa rangi Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |