Watu weusi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Martin Luther King, Mmarekani mweusi na mpiganaji wa haki za binadamu nchini Marekani.
Barack Obama, rais wa 44 wa Marekani, alikuwa Mwafrika Mmarekani wa kwanza kushika wadhifa huo.
Mwigizaji Rashida Jones hutazamiwa mtu mweusi pale Marekani kwa sababu baba yake ni Mwamerika mweusi
Watoto wa Visiwa vya Solomoni katika Melanesia ("Nchi ya watu weusi"), iliyopo kwenye visiwa vya Bahari ya Pasifiki
Mwanamume wa Kimasai nchini Kenya

Watu weusi ni msamiati unaotumika mara nyingi kumaanisha watu kutoka Afrika kusini kwa Sahara au watu wenye asili kutoka hapa.

Lakini si istilahi kamili kwa sababu kwanza kuna tofauti kubwa duniani ni watu gani wanaotazamwa kuwa "weusi" halafu kuna pia watu wenye rangi ya ngozi hiyo (nyeusi kiasi au ya kahawia) katika maeneo mbalimbali ya dunia, kuanzia India kusini kupitia Papua Guinea Mpya, Australia hadi Visiwa vya Melanesia ("visiwa vya Watu Weusi") katika Bahari ya Pasifiki, ambao wote hawana uhusiano na Afrika zaidi ya binadamu wote.

Halafu wako watu wengi wenye asili ya Afrika waliopelekwa Amerika kama watumwa tangu karne ya 16. Wengi wao wametokana kwa viwango tofauti na mababu ambako wakati fulani mabwana Wazungu walizaa na watumwa wa kike wenye rangi tofauti; ilhali watoto wa mama mtumwa alitazamiwa kuwa mtumwa hao wote walihesabiwa kama "watu weusi" hata kama urithi wa kimwili wa kizungu ulizidi urithi wa kimwili wa Kiafrika. Katika majimbo ya kusini ya Marekani (awali ya "shirikisho") ubaguzi wa rangi uliendelea vikali baada ya mwisho wa kisheria wa utumwa kwa kutenga kwa kuainisha wakazi wote kwa makundi ya "weupe" na "weusi"; hapa walitumia kanuni ya "One-drop rule (sheria ya "tone moja") iliyomwainisha mtu yeyote kuwa "mweusi" akijulikana kuwa na mhenga mmoja Mwafrika katika historia yake, bila kujali rangi yake halisi.[1][2]


Pamoja na hayo, siku hizi wengi wanaona msamiati huo si sahihi wala haina adabu, kwa jinsi unavyotumika.

Marejeo

  1. Davis, F. James. Frontline."Who's black. One nation's definition". Accessed 27 February 2015.
  2. Dworkin, Shari L. The Society Pages. "Race, Sexuality, and the 'One Drop Rule': More Thoughts about Interracial Couples and Marriage". Accessed 27 February 2015.