Melanesia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa Melanesia katika Pasifiki kaskazini ya Australia
Mwenyeji wa Vanuatu awafundisha watoto kutengeneza moto

Melanesia ni eneo la Bahari ya Pasifiki lililoko kaskazini kwa Australia. Ni mojawapo kati ya makundi makubwa matatu ya visiwa vya Pasifiki pamoja na Mikronesia na Polynesia.

Jina lake limeundwa na maneno ya Kigiriki μέλας cheusi na νῆσος kisiwa yaani "visiwa vyeusi" au zaidi "Visiwa vya Weusi". Nahodha Mfaransa Jules Dumont d'Urville alitunga jina hilo mwaka 1832 akitaka kutaja wazawa waliokuwa na rangi nyeusi-nyeusi.

Watu na utamaduni[hariri | hariri chanzo]

D'Urville alijumlisha wakazi wa visiwa hivyo pamoja kutokana na rangi yao. Lakini hali halisi ni watu wa aina mbalimbali. Wengine ni Waaustronesia, wengine Wapapua na wengine wametokana na mchanganyiko wa vikundi hivyo viwili.

Nchi za Melanesia[hariri | hariri chanzo]

Fiji, Papua Guinea Mpya, Visiwa vya Solomon, Vanuatu na Kaledonia Mpya (chini ya Ufaransa) zinajihesabu kuwa sehemu za Melanesia. Kuhusu visiwa vingine mawazo hutofautiana.

Visiwa vya Melanesia[hariri | hariri chanzo]

Visiwa na mafunguvisiwa vifuatavyo vinahesabiwa katika Melanesia:

Visiwa vilivyoko katika eneo hili lakini wakazi hawajitazami kuwa Wamelanesia:

Wakati mwingine hata visiwa upande wa Guinea Mpya vinahesabiwa humo ingawa wakazi hawajitazami hivyo: Halmahera, Alor na Pantar.

Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.