Historia ya Zimbabwe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Historia ya Zimbabwe inahusu eneo la Kusini mwa Afrika ambalo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Zimbabwe.

Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani.

Katika karne za kwanza BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi.

Tangu karne ya 11, Zimbabwe ya leo imekuwa na falme imara kwenye njia muhimu ya biashara.

Kampuni ya British South Africa ya Cecil Rhodes iliweka mipaka ya sasa katika miaka ya 1890.

Koloni la Uingereza lilianzishwa mwaka 1923 kwa jina la Southern Rhodesia.

Mwaka 1965, serikali ya walowezi Wazungu ilijitangazia uhuru kwa jina la Rhodesia tu.

Baada ya miaka 14 ya kutengwa kimataifa na kupigana na raia Waafrika katika miaka ya 1970, mapatano ya mwaka 1979 yalikubali wakazi wote wawe na haki ya kupiga kura na nchi ikawa huru kweli kwa jina la Zimbabwe mwaka 1980.

Rais Robert Mugabe alipata umaarufu katika siasa kama mpiganaji dhidi ya ukoloni lakini pia kama aina ya dikteta aliyerudisha nyuma uchumi wa nchi hadi alipolazimika kustaafu mwaka 2018.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Hourglass.svg Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Zimbabwe kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.