Washona

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Familia ya Shona

Washona ni watu wanaotumia lugha ya Kishona wanakaa hasa Zimbabwe pamoja nchi jirani.

Nchini Zimbabwe Washona ni takriban milioni 11 hivyo zaidi ya asilimia 80 za wananchi wote.

Mababu wa Washona waliunda milki kubwa kama Zimbabwe Kuu na Munhumutapa. Katika karne ya 19 wengi wao walifikishwa chini ya utawala wa Wandebele kutoka Afrika Kusini, kabla ya kuvamiwa na ukoloni wa Kiingereza.

Kati ya Washona mashuhuri wako Robert Mugabe, Emmerson Mnangagwa, na Morgan Tsvangirai.